Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalum Dk. Nandera Mhando akifungua kongamano la tisa la Aquarium 5$ kutoa matokeo ya utafiti lilioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na Hospital ya Taifa Muhimbili.
……………………………………
Jamii imeshauriwa kushirikiana na madawati ya kijinsia pamoja na mabaraza ili kuendelea kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanyika katika jamii yetu ili kuokoa wahanga wa matukio hayo.
Akizungumza katika uzinduzi wa Kongamano la tisa la Aquarium 5$ kutoa matokeo ya utafiti lilioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na Hospital ya Taifa Muhimbili Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalum Dk. Nandera Mhando amesema kuwa bado katika Jamii lipo ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Amesema hadi sasa asilimia 70 ya watoto na Wanawake bado wanafanyiwa vitendo vya ukatili ambapo Kauli mbiu ya kongamano Hilo ni “Kuzungumzia Changamoto za Ukatili na ugonjwa wa Afya ya akili ni wajibu wa tafiti na ujumuishi wa wadau mbali mbali”.
Serikali ipo katika maandalizi ya siku ya Afya ya akili duniani mbapo kongamano Hilo litaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto katika Jamii.
Ameeleza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliotolewa na Wizara ya Afya ulionyesha Afya duni ya akili imehusisha msongo wa mawazo na kutengwa na jamii
“Lengo la utafiti ni kutoa majibu ya Nini kifanyike ili kukabiliana na vitendo vya ukatili.
kwa sababu vitendo vya ukatili vina changamoto kubwa ya suala la aibu ikiwa ni pamoja na kujitenga na jamii,Kiwewe,Kisonona na wakati mwingine hupelekea kifo, ” Amesema Dk. Nandera Mhando
Amefafanua kuwa asilimia 10 ya watanzania walijaribu kama si kukusudia kujiuwa kutokana na changamoto ya Afya ya akili.
Amesema asilimia 12 ya watoto walijaribu kutaka kujiuwa kama sio kukusudia.
Amesema serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa kupata afua ya changamoto za ukatili.
na kwa sasa serikali imeazimia kuweka wasimamizi katika gari za shule ili kuhakikisha usalama wa mwanafunzi anaeanza kutoka katika gari na anayemaliza kushuka ili kuweka usalama wao wawapo njiani kwenda shule au kurudi nyumbani.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi, Muhimbili Prof.Bruno Sunguya. Akimkaribisha DK. Nandera Mhando ili kufungua kongamano Hilo.
Dkt.Omary Ubuguyu aliyemwamilisha Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya akizungumza Katika kikao hicho.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Utafiti na Ushauri, Prof Emmanuel Balandya akitoa neno la shukurani.
Picha mbalimbali zikionesha washiklriki wa kongamano Hilo wakifuatilia majadiliano.