Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini Tanzania –TMA Dkt Agnes Kijazi akizungumza katika Kongamano la 15 la wadau wa Satelite za hali ya Hewa za Shirika la EUMETSAT Barani Afrika ambao unafanyika kwa siku tatu linalofanyika kwenye ukumbi wa JNICC Posta jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete akufungua Kongamano la 15 la wadau wa Satelite za hali ya Hewa za Shirika la EUMETSAT Barani Afrika ambao unafanyika kwa siku tatu linalofanyika kwenye ukumbi wa JNICC Posta jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja
Picha zikionesha washiriki mbalimbali wa kongamano Hilo Kutoka nchi mbalimbali Afrika na Ulaya wakifuatilia majadiliano
Takriban Nchi 50 kutoka Afrika wameshiriki katika mkutano Mkuu wa watumiaji wa taarifa kutoka kwenye satelaiti za Hali ya Hewa ili kuangalia faida wanazozipata kutoka katika satellite hizo.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika Kongamano la 15 la wadau wa Satelite za hali ya Hewa za Shirika la EUMETSAT Barani Afrika ambao unaofanyika kwa siku tatu,Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete amesema Serikali itaendelea kufunga rada katika maeneo mbalimbali ili kufanya urahisi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kufanya kazi zake Kwa ufanisi.
Naibu Waziri ameipongeza serikali kwa kuendelea kuongeza rada zitakazosaidia katika ufanisi wa TMA kwa kutoa taarifa kwa wakati za Hali ya Hewa na hivyo kuwafanya wananchi kuufahamu umuhimu wa Utabiri ulio sahihi.
Aidha amesema kuwa serikali itakwenda kufunga rada katika mikoa mbalimbali hasa ya Nyanda za Juu kusini ukiwemo Mkoa wa Kigoma lakini pia rada nyingine zipo kwenye matengenezo na zitakapokamilika zitafungwa.
Rada tatu zimefungwa tayari na mbili zimekamilika tutaanza kufunga wakati wowote kuanzia sasa lakini pia mbili zipo kiwandani kwenye matengenezo na zote Mhe Rais ameshalipa fedha’amesema Naibu Waziri Mwakibete
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini Tanzania –TMA Dkt Agnes Kijazi amesema katika mkutano huo pia wanaangalia faida na changamoto zilizopo ili waweze kuziboresha.
Amesema kuwa Sateline inaona kutoka angani na kuangalia maeneo yote ya nchi hivyo inatoa msaada mkubwa kwa taarifa za hali ya hewa kwa ajili ya kutoa utabiri.