Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhudhuria hafla ya uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. William Samoei Ruto.
Aidha, Rais Samia atahudhuria uapisho huo wa Rais Ruto
utakaofanyika jijini Nairobi kesho tarehe 13 Septemba, 2022.
Rais Samia ataambatana na baadhi ya Viongozi wa Serikali
akiwemo Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Mhe. Harusi Said Suleiman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
ZuhuraYunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu