Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza miliki wa kiwanda cha Zanzibar Handmade Cosmetics Shekha Nasser wakati akiangalia Bidhaa katika mabanda mbalimbali ya Maonesho kabla ya kuhutubia viongozi mbalimbali wa Ndani na Nje ya Nchi kwenye Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam tarehe 12 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan akimsikiliza miliki wa kiwanda cha Zanzibar Handmade Cosmetics Shekha Nasser wakati akiangalia Bidhaa katika mabanda mbalimbali ya Maonesho kabla ya kuhutubia viongozi mbalimbali wa Ndani na Nje ya Nchi kwenye Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam tarehe 12 Septemba, 2022.
Mmiliki wa kiwanda cha Zanzibar Handmade Cosmetics Shekha Nasser akiwapa maelezo wateja waliotembelea na kuangalia Bidhaa katika banda lake na mabanda mbalimbali ya Maonesho kwenye Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam tarehe 12 Septemba, 2022.
Zainab Anselll Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Zara Tours akiangalia bidhaa za vipodozi vya kiasili kwenye banda la kiwanda cha Zanzibar Handmade Cosmetics huku akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa kiwanda hicho Shekha Nasser.
DAR ES SALAAM.Mazao ya Mwani na Mdalasini yametajwa kuwa sehemu ya mazao muhimu nayoweza kubadilisha uchumi wa wananchi wa Zanzibar katika kuendeleza Sera ya uchumi wa Buluu Visiwani humo.
Hayo yamebainishwa na mmiliki wa kiwanda cha Zanzibar Handmade Cosmetics Shekha Nasser alipozungumza katika mahojiano maalum kwenye Kongamano la wanawake na vijana wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) linalofanyika kwenye ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.
Shekha amesema kuwa kutokana na fursa pana zilizopo kwenye zao la Mwani na Mdalasini wamekuwa wakifanyakazi ya kuyaongezea dhamani mazao hayo kwa kuyabadirisha na kuiunga kwenye sabuni na katika bidhaa nyingine ambazo zimekuwa zikipendwa na watu wengi.
“Tunaamini kwa kuongeza thamani kilimo cha mwani kitaongezeka kwa sababu tutakuwa tunanunua mwani kutoka kwa wakina mama wanaolima mwani ili kutengeneza sabuni” amesema Shekha.
Ameongeza kuwa “bidhaa zetu zinakwenda sana kwa sababu ni za asili, lakini sasa hivi pia tunanunua bidhaa za Cocoa Butter na na mafuta mengine kutoka mikoani ikiwemo iringa, lindi na Rufiji mafuta ya nazi” ameongeza.
Hata hivyo amesema kuwa pamoja na jitihada hizo wanashindwa kushindana na viwanda vikubwa kutokana na viwanda vivyo kununua malighafi nje ya nchi kwa bei ya chini tofauti na wao ambapo wanalazimika kupata malighafi hizo hapa hapa nchini kwa gharama kubwa.