…………………….
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameihakikishia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii kuwa Wizara anayoiongoza itaendelea kushirikiana na Wizara nyingine za Kisekta katika kuboresha mipaka ya Hifadhi za Taifa pamoja na shughuli za uhifadhi na Utalii kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.
Waziri Balozi Dkt Chana ameyasema hayo katika kikao cha Kamati hiyo ya Bunge na Kamati maalum ya Mawaziri nane wa kisekta inayoshughulika migogoro ya Ardhi nchini.
Waziri Balozi Dkt. Chana amewashukuru wajumbe wa Kamati hiyo kwa michango muhimu ya kuboresha shughuli za Maliasili na Utalii pamoja na usimamizi na uboreshaji wa mipaka ya Hifadhi za Taifa nchini.
Kamati hiyo ya Mawaziri nane inajumuisha Mawaziri kutoka Maliasili na Utalii, Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, TAMISEMI, Waziri wa Maji, Mifugo na Uvuvi, Waziri Ulinzi, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na Waziri wa Fedha.