CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA)kimepongeza uteuzi wa mmoja wa wanachama wake katika Baraza la Taifa la Usalama Barabarani uliofanywa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Massauni.
Aidha katika kutia mkazo dhidi ya suala hicho, Chama hicho kwa makubaliano ya wanachama wake wote kimesema kuwa kitaandikia barua rasmi kwenda kwa Waziri Massauni kuelezea kufarijika kwao na uteuzi huo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa chama hicho Abdallah Kiongozi pamoja na mambo mengine amesema wao kama wadau muhimu katika sekta ya usafirishaji nchini, uteuzi huo umewafanya waone kuwa mchango wao katika Serikali unatambulika.
Awali wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya Ndani Waziri Massauni alifanya uteuzi wa MwenyekitiMwenyekiti, Makamu Mwenyekiti pamoja na wajumbe 18 wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambapo miongoni wa wajumbe hao yupo Mweka Hazina wa TABOA ISSA Nkya.
Uteuzi wa wajumbe hao unaongozwa na Mwenyekiti wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, Makamu wake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Atupele Mwakibete huku jina la aliyekuwa Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Taifa Mohammed Mpinga nalo likichomoza miongoni mwa majina ya wajumbe.
” Tumevutiwa na uteuzi wa mmoja wa wajumbe wetu katika Baraza la Usalama. barabarani, sisi kama wamiliki ni sehemu ya watumiaji wakubwa wa huduma za barabara, tunaamini uwepo wa mjumbe huyu kutachangia kupata mawazo yenye tija kwa maendeleo na usalama katika sekta ya usafiri wa barabara” amesema Kiongozi.
Kwa mujibu wa kifungu cha 97 Cha Sheria za Usalama Barabarani, miongoni mwa kazi za Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ni pamoja na kusimami shughuli zote za kuhimarisha usalama barabarani na kutumia maarifa na uzoefu uliopo kuhusu usalama barabarani.
Majukumu mengine ni kuhamasisha tafiti kuhusu vyanzo vya ajaliajali, kuhamasisha tafiti kuhusu idadi,aina na gharama zitokanazo na ajali za barabarani hapa nchini.