Katibu Itikadi na uenezi Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba kuhusu maazimio ya kika Cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Jana jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu Hassan.
Waandishi wa Habari wakimsimiliza Katibu Itikadi na uenezi Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka.
………………………………
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba Dar es salaam Katibu Itikadi na uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka amesema kwamba Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa imekutana katika kikao chake maalum (Jana) Jumatano tarehe 07 Septemba, 2022 chini ya Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu Hassani.
Aidha amesema kuwa kamati kuu hiyo baada ya kutafakari na kijadiliana Kwa kina imeona kuwa kuna umuhimu wa serikali kusikiliza maoni na ushauri wa wananchi Kuhusu Utekelezaji wa bajeti hiyo hususani katika eneo la tozo za miamala ya kielekroniki iliyoanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2022/2023.
“Kuhusu suala hili la tozo ,nawaomba Wananchi waendelee kuwa na imani na serikali yao,serikali inalifanyia kazi suala hili na itachukua hatua stahiki baada ya kusikiliza maoni na ushauri kutoka kwa wananchi ” amesema Shaka.
Amendelea kusema kuwa pamoja na Mambo mengine Kamati Kuu ya CCM imepokea na kujadili taarifa kutoka vitengo vya chama kuhusu utekelezaji wa kazi za chama na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“Baada ya kujadili kwa kina kamati kuu imefikia maamuzi ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kwa namna anavyoendelea kuiongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutafsiri kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 –2025, katika kuimarisha huduma za kijamii, kuimarisha ustawi wa wananchi, kukuza uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja ikiwa ni kushamirisha na kuharakisha maendeleo endelevu” amesema.
Aidha Katibu huyo Mwenezi wa CCM Taifa amebainisha kuwa miongoni mwa maeneo muhimu na yaliyopewa kipaumbele ni Sekta ya Kilimo ambapo kupitia Bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023, imeweka msukumo mkubwa katika kuboresha kilimo kwa kutenga bajeti kiasi cha shilingi bilioni 954 ikiwa ni ongezeko la 224%.
Amesema kuwa serikali imetambua kilimo cha kisasa kitachangia Kwa kiasi kikubwa kuongeza ajira, kipato cha wakulima,kuwezesha nchi kujitosheleza kwa chakula, kuimarisha uzalishaji na uchumi wa nchi.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea, kutafakari na kujadili kwa kina kuhusu hatua za kibajeti zinazoendelea kuchukuliwa kwa lengo la kupata fedha za kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kasi ili kuwawekea wananchi mazingira mazuri ya kujipatia maendeleo, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025.
Aidha amebainisha kuwa eneo moja wapo ni Tozo ambapo serikali imeweza kufanya mambo makubwa katika kipindi kifupi akitolea mfano ujenzi wa vituo vya afya 234 na shule mpya za sekondari 214 na maeneo mengine kadhaa ambayo yanagusa maisha ya watanzania ya kila siku.