NA. MWANDISHI WETU JESHI LA POLISI
Jeshi la Polisi Tanzania linapenda kuwafahamisha watanzania kuwa Mwenyeji wa Michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika, awamu ya Kumi na Moja (11) (11th Ed SARPCCO GAMES) iliyoanza kufanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 04 – 17 Septemba 2022.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura anapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa, tarehe ya kufunguliwa rasmi michezo hiyo imesogezwa mbele badala ya kufanyika tarehe 10 Septemba 2022 siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi
Aidha SACP Misime amesema kuwa Katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo, mgeni rasmi atakuwa Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Michezo inayoshindaniwa ni pamoja na mpira wa miguu (football) (wanaume na wanawake), mpira wa pete (netball) (wanawake), mpira wa wavu (volleyball) (wanawake na wanaume), tennis (wanawake na wanaume), vishale (darts) (wanaume na wanawake), riadha (wanawake na wanaume), pamoja na chess (wanawake na wanaume).
Sambamba na hilo SACP DAVID MISIME amesema Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, anawaalika wanahabari na wananchi wote kwa ujumla kuja kushuhudia ufunguzi rasmi wa michezo hiyo katika Uwanja wa Uhuru, pia kila siku kuna michezo inayoendelea kuanzia asubuhi hadi jioni katika viwanja nilivyovitaja hapo juu. Aidha hakuna kiingilio chochote katika kuona michezo hiyo na ufunguzi huo.