Mkurugenzi wa huduma za Taasisi (DCS) Bw. Immanuel I Mgonja (watatu kushoto) akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu na Uendelezaji tafiti (DRCP), Dkt Paul Ochang’a (wakwanza kushoto) akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusuiano Kimataifa IOP, Dominic Hurley (wapili kushoto), Msimamizi wa mradi wa FSBL Tanzania, Bi. Linsey Simkin (watatu kulia), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa IOP Bi Rachel Youngman (wanne kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Atamizi ya DTBI, Dkt Erasto Mlyuka (wapili kulia) , Meneja Mradi wa FSBL, Bi. Josephine Sepeku (wanne kulia) na Meneja Biashara wa Atamizi ya DTBI, Bw. Elia Kinshaga mara baada ya kupokea ujumbe huo – Sayansi (Kijitonyama) – Jijini Dar es salaam
……………………..
COSTECH-Dar es salaam
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imepokea ujumbe tarehe 6 septemba 2022 kutoka Chuo Kikuu cha Fikizia cha nchini Uingereza wenye lengo la kutembelea mradi wa FSBL (Future STEM Business Leader) unaowajengea uwezo walimu na wanafunzi katika masomo ya Sayansi, Teknolokojia, Hisabati na Uhandisi nchini, Ujumbe huo umepokelewa kupitia ukumbi wa Mikutano COSTECH uliopo katika Ofisi za Tume – Sayansi (Kijitonyama) – Jijini Dar es salaam
Akizungumza wakati akifungua kikao hicho, Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (DCS) kutoka COSTECH, Bw. Immanuel I. Mgonja alisema wanafunzi wengi wamekuwa hawavutiwi na masomo ya Sayansi ikiwemo somo la fizikia (Physics) kwasababu ya kuwepo kwa changamoto ya ufundishaji wa walimu kwa njia ya nadharia zaidi kuliko vitendo.
“kumekuwa na changamoto ya baadhi ya walimu kukosa ubunifu na mifano hai wakati wa ufundishaji, hivyo hupelekea Vijana wengi kutokuwa na muamko wa kusoma masomo ya Sayansi ikiwemo fizikia ni kutokana na uchache wa walimu na vifaa vya kufundishia katika sekta ya elimu’’ Bw. Mgonja aliongeza
Ujumbe huo unatarajia kuanzisha mpango wa miaka 5 wa ufadhili Kiasi cha Euro Milioni E20 – E25 sawa na Tsh. Bilioni 57 za Kitanzania, mpango wa ushirikiano huo wa Afrika na nchi za Jumuiya ya Madola wa kifizikia kupitia programu AUPP (Afrika – UK Physics partnership) utakaotembelea nchi tano (5) za Afrika ili kuibua watafiti wachanga na wenye vipaji waweze kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi (hali ya hewa) na nishati mabadala ikiwemo Taifa la Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika Kusini na Rwanda.
Akifafanua zaidi kuhusu msimamizi wa mradi wa FSBL Tanzania, Meneja Uhusiano wa Kimataifa IOP, Bi. Linsey Simkin amesema ni muhimu kuendeleza juhudi za kuchochea wanafunzi kupenda masomo ya STEM yahayosimamiwa na Atamizi ya DTBI iliyopo chini ya COSTECH. Bi Linsey aliambatana na Mkuu wa Kitengo cha Uhusuiano wa Kimataifa , Bw. Dominic Hurley Pamoja na Makamu Mkurugenzi Mtendaji (Deputy CEO) kutoka Idara ya Fizikia ya Uingereza (IOP).
Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu na Uendelezaji wa Tafiti (DRCP) toka COSTECH Dkt. Paul Ochang’a aliwakabidhi wajumbe Muongozo wa Kitaifa wa Vipaumbele vya Utafiti na kuongeza kuwa COSTECH iliandaa mwongozo huo kupitia ukurasa wa 19 unazungumzia sekta izo mbili za ya nishati mbadala (Renewable Energy) na Mabadiliko ya tabia ili kutoa hamasa na nafasi kwa wadau wa Tume kushiriki katika kujenga uwezo wa watafiti wachanga, mashirikiano na miundombinu ya uendeshaji tafiti nchini.
Dkt. Paul anafafanua kumekuwa na uwoga kwa wanafunzi wa kike kuchukua masomo ya Sayansi jambo linalopelekea kukosekana kwa usawa wa kijinsia katika ufundishaji wa somo husika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Atamizi ya DTBI, Dkt Erasto Miyuka, alisema Tume imeweka mazingira wezeshi kupitia Mfuko wa Taifa Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) ambayo kazi yake ni kupokea fedha za wafadhili wa ndani na nje na kusimamiwa matumizi yake.
Kwa upande wake, Meneja Mradi wa FSBL inayoratibiwa COSTECH chini ya atamizi ya DBTI iliyopo chini ya COSTECH, Bi. Josephine Sepeku alifafanua kuwa mafanikio yatokanayo na mradi huo kwasasa ni mzuri kwani ulianza na jumla ya shule sita (6) na sasa umefikia jumla ya shule 17 pamoja na kuongeza wigo na wabia wa mradi ambapo ulianzishwa Mkoani Dar es salaam pekee na kwasasa umefikia Mkoa wa Arusha