Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, ametia saini kitabu cha wageni katika Ofisi za CCM Mkoa wa Geita na kuzungumza na viongozi wa Chama wa mkoa huo.
Kinana akizungumza na viongozi hao, amewataka kuendeleza ushirikiano uliopo ambao amesema ni nyenzo muhimu na msingi sahihi kwa maendeleo ya jamii.
Pia, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na viongozi Kwa Ushirikiano wa Chama na serikali mkoani humo huku akiwasisitiza viongozi na watendaji kuendelea kutatua changamoto za wananchi ili kuharakisha maendeleo.
Kinana aliyeambatana na Katibu wa Halashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, yuko mkoani Geita kwa ajili ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.