……………………….
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya Usimamizi na Uendelezaji wa rasilimali za Maliasili na Utalii.
Akizungumza wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii na Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe Juma Ally Makoa (MB), amesema Juhudi zilizo anzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kusimamiwa kikamilifu na Wizara ya Maliasili na Utalii za kulinda na kuendeleza Hifadhi ya Ngorongoro zinapaswa kupongezwa na kuungwa mkono na Watanzania wote kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Wizara anayoiongoza itaendelea kusimamia kwa weledi mkubwa na kwa mujibu wa sheria uhifadhi endelevu wa Maliasili na Utalii ili rasilimali hizo ziweze kuwanufaisha watanzania wote.