Makamu Mwenyekiti wa ccm Tanzania bara comrade Abdulrahman Kinana ametoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya wakulima pale wanapotaka kuuza mazao yao.
Akizungumza na wana CCM na wananchi waliyojitokeza kumlaki Wilayani Muleba mkoani Kagera, Kinana amesema nia ya mkulima na mfanyakazi ni kuondokana na umasikini na siyo kukutana na vikwazo.
“Watu wanalima wanafanyakazi ili kuondokana na umasikini hawataki vikwazo. Wakati wa kulima hatuwasaidii, wakati wa kupalilia hutuwasaidii, wakati wa kuweka dawa hatuwasaidii,wanapokwenda kuvuna hatuwasaidii, wakishavuna wanataka kuuza na sisi tuko hapo. Sasa shamba lako langu.. kahawa yako yangu! Kama kahawa ni yangu nitamuuzia atakayenipa bei nzuri “ alisema Kinana huku akishangiliwa.
Kinana amemuomba mkuu wa mkoa wa Kagera kuwalinda wakulima wanapotaka kuuza kahawa yao nje.
“ Nataka nikuhakikishie ndugu mkuu wa mkoa tutakulinda.Hakuna kahawa ya magendo nisikilizeni hakuna kahawa ya magendo. Kahawa yangu nikiuza popote kwa yoyote itakuwaje magendo?” AlisemaK
inana akiongozana na katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka katika ziara hiyo iliyoanzia Kigoma ambapo Jumamosi anatarajiwa kuelekea Geita kabla ya kumaliza katika mkoa wa Mwanza kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.