Meneja wa Mawsiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta (watano kulia) akikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo Unga, sukari ,mafuta maziwa, mchele na vinginevyo kwa Mkuu wa Kitengo cha Wanafunzi wenye ulemavu wa akili kilichopo katika shule ya msingi Bunju B, jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Afisa Masoko wa Benki hiyo Dorothea Lymo, watoto pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa kituo hicho Asaph Marere. Hafla hiyo imefanyika leo shuleni hapo.
Afisa Masoko wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Dorothea Lymo, akikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo Unga, sukari ,mafuta maziwa, mchele na vinginevyo kwa Mwenyekiti wa kituo hicho Salehe Athuman cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili katika shule ya msingi Bunju B, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Mawsiliano na Uhusiano waTanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta, uongozi wa kituo hicho pamoja na wanafunzi hao hafla hiyo imefanyika leo shuleni hapo.
Meneja wa Mawsiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta (watatu kulia), akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Wanafunzi wenye ulemavu wa akili kilichopo katika shule ya msingi Bunju B, Gloria Mataba, wakati wa hafla ya benki ya TCB ilipokwenda kutembelea kituo hicho nakutoa misaada ya vitu mbalimbali vya kibinadamu. Wengine pichani ni Mkuu wa kituo msaidizi Asaph Marere pamoja na wanafuzi hao.
Meneja wa Mawsiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta (wanne kulia), pamoja na Meneja Masoko wa Benki hiyo Dorothea Lymo wakiwaraki watoto wenye ulemavu wa akili wanaolelewa katika kituo kilichopo ndani ya shule ya msingi Bunju B walipokwenda kuwatembelea na kuwapa msaada wa mahitaji mbalimbali.