Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMA) Dkt Agnes Kijazi akifungua semina ya waandishi wa habari kuhusu utabiri wa mvua za Vuli unaotarajiwa kufanyika jumatano Septemba 2 jijiinDar es Salaam iliyofanyika kwenye kituo chautafiti wa kilimo TARI Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMA) Dkt Agnes Kijazi akimsikiliza Meneja Kituo Kikuu cha utabiri ndani ya Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA, Samwel Mbuya wakati akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika semina hiyo.
Mchambuzi wa Hali ya Hewa Mamlaka ya Hali ya Hewa Bi Rose Senyagwa akiwa makini wakati mambo mbalimbali yakijadiliwa katika semina hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa wakifutilia mijadala katika semina hiyo
Waandishi mbalimbali wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Mchambuzi wa Hali ya Hewa Mamlaka ya Hali ya Hewa Bi. Rose Senyagwa akifafanua jambo wakati mambo mbalimbali yakijadiliwa katika semina hiyo.
Picha ya pamoja.
………………………………..
Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini -TMA imewataka waandishi wa habari Nchini kuendelea kuandika taarifa zinazohusiana na Hali ya Hewa Kwa usahihi Ili kuisaidia Jamii kupata uelewa katika nyanja mbalimbali kupitia taarifa Hizo
Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMA) Dkt Agnes Kijazi ameeleza hayo mkoani Pwani wakati akifungua warsha ya wanahabari kuhusu kuelekea kutolewa kwa utabiri wa Mvua za Vuli zinazotarajiwa kuanza Mwezi Oktoba mpaka Disemba Mwaka huu ambayo wameipa Mbiu isemayo Matumizi sahihi ya taarifa za Hali ya Hewa Kwa Maendeleo endelevu
Dkt Kijazi amesema kuwa taarifa ambazo wanazitoa zikizifikia kwa wakati Mamlaka inasaidia kuweza kukabiliana na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza yanayosababishwa na Mabadiliko ya Hali ya Hewa.
Aidha Mkurugenzi Huyo amewakumbusha wanahabari nchini kuendelea kuwa mabalozi wazuri kwa kuwaelezea wananchi sehemu wanayopaswa kupata taarifa sahihi ya Hali ya Hewa kuwa ni TMA pekee.
“Kwa kushirikiana na nyie wanahabari vizuri na mukaweza kufikisha taarifa kwa wananchi basi wananchi wataweza kujua ni taarifa gani ambayo wataitumia Kwa Muda na wakati sahihi “amesema Dkt Kijazi
Amesema vyombo vya habari Tanzania ni namba Moja katika kutoa taarifa za Nchi na hivyo kuwasaidia watanzania kupata uelewa Mkubwa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa yanayojitokeza.
Dkt Kijazi amesema nyakati za sasa kumekuwa na Muamko Mkubwa kwa wananchi kuzifahamu taarifa za Hali ya Hewa na hivyo kufahamu namna ya kupambana na changamoto Katika Mazingira Yao.
Hata hivyo amesema kuhusu utabiri wa Mvua za Vuli zinazotarajiwa kuanza Mwezi Oktoba mpaka Disemba unatarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa Septemba 2 Mwaka huu.