RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kupewa mkono wa pole na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Mhe. Zito Zuberi Kabwe, wakati wa maziko ya Kaka yake Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi yaliyofanyika Kijiji kwao Mangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja leo 31-8-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Siasa katika Sala ya Jeneza ya Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Kaka yake iliyofanyika Kijijini kwao Mangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja leo 31-8-2022, na (kulia kwa Rais) Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi,Mbunge wa Jimbo la Mahonda Mhe. Abdalla Hassan Mwinyi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Alhaj Zuberi Ali Maulid .(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi ikisomwa na Sheikh Shariff (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Mangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja leo 31-8-2022 na (kushoto kwa Rais) Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Hemed Abdulla Suleiman na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dkt.Amani Karume.(Picha na Ikulu)
RAIS Mstafu wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Mtoto wake Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi maziko yaliofanyika leo 31-8-2022 Mangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja leo 31-8-2022.(Picha na Ikulu)