………………….
NA MUSSA KHALID
Nyumba moja iliyopo Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam imeteketea kwa moto asubuhi ya leo chanzo kikidaiwa ni hitilafu ya umeme.
Wakizungumza na Kituo hiki wapangaji wa nyumba hiyo Mahadike Willium pamoja na Vicent Fransis wamesema tukio hilo limesababisha kutetekeza vitu vyao muhimu vilivyokuwepo katika vyumba vyao.
‘Chumba changu huwa kunashoti hivyo umeme ulivyorudi kwa kasi nadhani shoti ikatokea na kusababisha kuungua chumba changu na kuhamima kwa vyumba vya wapangaji wenzangu na wakati huo nilikuwa mimi nimetoka niliporudi nilikuta kila kitu kimetekea kwa moto vikiwemo vyeti vyangu na nguo zangu’ameelezea Mahadike
Mmiliki wa Nyumba hiyo Bi Saita Mwakisyala amesema alipata taarifa ya kuungua kwa nyumba hiyo kutoka kwa mpita njia lakini hata hivyo walivyojaribu kuwapigia TANESCO na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mawasiliano yao hayakupatikana kwa wakati.
Bi. Saita amesema kuwa baada ya kufanikiwa kuwapata na walipofika bado miundombinu ya kuingiza gari kwenda kuzima moto ikawa ni changamoto hivyo moto huo ukaendelea kutekeza nyumba hiyo.
Naye Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Jaffary Juma Nyaigesha amesema tukio hilo limeanza wakati umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara huku akieleza pia kutokuwa na miundominu rafiki ya maeneo hayo imesababisha moto huo kutokuzimwa kwa wakati na magari ya kuzimia moto.
Kwa upande wao Afisa habari wa Jeshi la Zimamoto Kinondoni Sajent Aman Hassan pamoja na Meneja TANESCO Wilaya ya Kitanesco Kimara Jamali Kimolo wamesema kuwa baada kupata taarifa ya moto huo wamefika eneo la tukio na kuudhibiti lakini pia bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini hasa chanzo chake.
Hata hivyo Diwani wa Kata ya Ubungo ambaye ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo ameitisha Kikao cha wananchi siku ya Kesho jioni kwa lengo la kujadili namna ya kuwasaidia wahanga wa tukio hilo.