……………..,……..
Na Sixmund J. Begashe wa MNRT
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), imepongezwa kwa juhudi inazochukua za kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuimarisha mifumo ya utendaji kazi, usimamizi wa rasilimali na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Pongezi hizo zimetolewa leo Agosti 29, 2022 na Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt. Pindi chana wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Makamanda na Wakuu wa vituo mbalimbali vya TFS Jijini Dodoma.
Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana amemshukuru, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais Mhe. Philip Mpango na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahimiza wananchi kupanda miti na kuitunza akisisitiza kuwa juhudi za viongozi hao wakuu zinapaswa kuungwa mkono na kila mwananchi.
“Nawaelekeza muendelee kusimamia sheria, wavamizi wote wasipewe nafasi na pale ambapo tayari wapo wavamizi shirikianeni na Kuu za mikoa na wilaya kuhakikisha wavamizi wote wanaondoka na kuacha hifadhi za misitu zikiwa salama”. Ameongeza Mhe. Balozi Dkt. Chana