Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (Mbunge) amezindua rasmi mradi wa urejeshaji Mto Nduruma kwenye mkondo wake ili kunusuru makazi 730 yaliyokuwa yakiathiriwa na mafuriko katika Kata za Shambarai Burka na Mbuguni, pamoja na hekari 3,280 za mashamba na barabara 5 zenye jumla ya urefu wa Km 18.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo uliofanyika katika Kata ya Shambarai burka Mhe.Waziri Aweso amesema Serikali ya awamu ya Sita ikiongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan inahakikisha wananchi wake wapo salama kwani imetoa milioni 250 za mradi huo wa kurejesha Mto kwenye mkondo wake ili kudhibiti mafuriko “Serikali ilisikia kilio chenu na kuleta fedha hizi, nitoe wito kwenu kutokufanya shughuli au kuharibu vyanzo vya maji kwani jukumu la kutunza vyanzo vya maji ni jukumu letu sote ” amehimiza Mhe. Aweso
Mhe. Aweso amesema wananchi na viongozi hawana budi kutunza vyanzo vya Maji kwani maji hayana mbadala na kwakuwa ni uhai hakuna uhai bila maji ambapo amewaagiza Wakurugenzi wa Mabonde yote ya maji nchini