Mratibu wa Huduma za Kutokomeza Trakoma (Vikope) kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTD) Bw. Ambakisye Mhiche aeleze hali ya ugonjwa wa vikope nchini na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030.
Pia, amewataka wananchi kuunga mkono jitihada hizo ili kufikia malengo ya Serikali baada ya kusainiwa kwa azimio la Kigali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Januari 27, 2022.