…………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amezindua rasmi Programu ya mafunzo yanayolenga kuImarisha huduma kwa wadau walio katika mnyororo wa huduma za Utalii inayoendeshwa na Chuo Cha Taifa cha Utalii (NCT) nchini.
Programu hiyo iliyozinduliwa leo na kufadhiliwa na Bank ya NMB inawahusu maafisa uhamiaji kama wadau muhimu watakaofaidika na mafunzo hayo katika mikoa yenye malango makuu ya kuingilia watalii nchini yaani Dar es salaam, Zanzibar na Arusha na Kilimanjaro ambapo takribani maafisa 700 wa uhamiaji watanufaika na programu hiyo.
Licha ya kuishukuru Benki ya NMB kwa mchango wake mkubwa, Waziri Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana ametoa wito kwa wadau wengine wa Utalii kujitokeza kuunga Mkono Juhudi za Serikali chini ya Mhe Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuendeleza sekta ya Utalii kwa maslai mapana ya watanzania wote
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt.Shogo Mlozi, amesema wanakusudia kuwafikia wadau zaidi ya 5,000 kutoka Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Mara na mikoa mingine ya Tanzania kwa kuwa maeneo hayo yanahuduma nyingi za Kitalii.