Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine Shilogile (kushoto) akizungumza na Mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu THRDC Onesmo Olengurumo katika mafunzo ya ujengaji uwezo kwa maafisa wa polisi, waendesha mashtaka na watendaji dawati la jinsia katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel Jijini Dar es Salaam, yakiwahusisha maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga.Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine Shilogile akizungumza katika mafunzo ya ujengaji uwezo kwa maafisa wa polisi, waendesha mashtaka na watendaji dawati la jinsia katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel Jijini Dar es Salaam, yakiwahusisha maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga.Mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu THRDC Onesmo Olengurumo akizungumza katika mafunzo ya ujengaji uwezo kwa maafisa wa polisi, waendesha mashtaka na watendaji dawati la jinsia katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel Jijini Dar es Salaam, yakiwahusisha maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga.Picha ya pamoja
……………………
NA MUSSA KHALID
Wakuu wa upelelezi wa mikoa pamoja na madawati ya jinsia nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa karibu upelelezi wa kesi za ukatili wa kijinsia ili kukamilisha ushahidi wa kesi hizo na hatua ziweze kuchukuliwa.
Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine Shilogile ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika mafunzo ya ujengaji uwezo kwa maafisa wa polisi, waendesha mashtaka na watendaji dawati la jinsia mafunzo ya kushughulikia kesi za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.
Amesema changamoto iliyopo ni kuwa kesi hizo zimekuwa zikiachwa kwa watendaji wa madawati ya jinsia kusababisha kutokamilika kwa ushahidi.
Aidha Kamishna Shilogile amesema kuwa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yamekuwa yakiongezeka hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kuzipata mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana nazo.
“Jeshi la Polisi pamoja na wadu wengine wa haki jinai Tunaendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na matukio haya lakini pia kuahidi ushirikiano ili kuhakikisha jamii yetu inakuwa kwenye usalama kutokana na matukio hayo”amesema Kamishna Shilogile
Kwa upande wake Mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu THRDC Onesmo Olengurumo amesema mafunzo hayo yatasaidia ni kujenga umoja katika ya vyombo vya usalam na watetezi wa haki za binadamu kuboresha hali ya haki za binadamu nchini.
Amesema kuwa ili kufanikisha kukabiliana na changamoto hizo ni vyema wadau wote wakashirikiana kwa pamoja wakiwemo wananchi ili kuhakikisha haki zinalindwa.
Amesema mafunzo hayo yanalenga kukumbushana kuhusu misingi ya haki za binadamu na kujadili changamoto zilizopo hususani za ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili wa watoto ili kushauriana namna bora ya kuzitatua.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Mkurugenzi msaidizi ofisi ya taifa ya mashtaka Renatusi Mkude amesema ipo haja kwa watendaji wa vyombo vya haki jinai kupewa mafunzo lengo ni kubadilishana uzoefu ili kutorudia makosa yanayofanyika.
Mafunzo hayo yanafayika kwa siku mbili yameanza leo Augosti 17, 2022 katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel Jijini Dar es Salaam, yakiwahusisha maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga.