Afisa masoko kutoka kampuni ya Epinav Agricultural Solutions, Gerald Chilebenje akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha huku akionyesha kombe baada ya kuibuka washindi wa pili kwa wasambazaji wa mbegu katika maonyesho ya nanenane mwaka huu. Moja ya mbegu za nyanya ambazo zimekuwa zikipatikana kutoka kampuni hiyo ya Epinav .
………………..
Julieth Laizer, Arusha.
Arusha.Wakulima wameshauriwa kutumia mbegu zinazostahimili ukame na kuzuia magonjwa ya mnyauko na kuweza kufanya kilimo biashara kwa kuvuna mavuno mengi na yenye ubora.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Afisa masoko wa Kanda ya kaskazini kutoka kampuni inayojihusisha na uuzaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbegu za mbogamboga ya Epinav Agricultural Solutions Ltd, Gerald Chibelenje wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Chibelenje amesema kuwa,wamekuwa wakiuza mbegu bora zinazostahimili ukame na kuzuia magonjwa ya mnyauko ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa wakulima hususani katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Amesema kuwa,wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara kwa wakulima namna bora ya kulima kisasa na kuweza kuvuna mazao mengi zaidi na kuweza kuwaongezea kipato.
“mbegu zetu zimekuwa zikistahimili Sana ukame na kuweza kulimwa katika mazingira yoyote ,hivyo tunawaomba wakulima watumie mbegu zetu Kwa kilimo biashara na kilimo bora ambacho kitawasaidia kujikwamua kiuchumi kwa ujumla.”amesema
Aidha amefafanua kuwa wameweza kushiriki katika maonyesho ya nanenane mwaka huu kwa mara ya kwanza ambapo wameweza kuwa washindi wa pili kwa makampuni yanayouza mbegu na kuweza kupewa kombe .
Ameongeza kuwa, wamekuwa wakiuza mbegu za nyanya,hoho,kabeji,na wana udongo wa kuoteshea mbegu,pamoja na mfumo wa umwagiliaji wa matone ,na mabomba ya mgongoni aina ya (solo) kutoka Ujerumani.
Nao baadhi ya wakulima wanaotumia mbegu hizo ,Aneth Misha amesema kuwa, mbegu hizo zimekuwa msaada mkubwa Sana kwao kwani zimekuwa zikistahimili ukame na kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuweza kuzalisha mazao mengi .
Aidha amewataka wakulima kutumia mbegu hizo kwani ni bora na zinakabiliana na ukame na kuweza kuvuna mavuno mengi zaidi.
Mwisho.