Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amehimiza watanzania wajitokeze kuhesabiwa Katika zoezi la sensa ya watu na makazi,kwani zoezi Hilo ni muhimu katika upangaji wa maendeleo ya nchi. Aidha amesema takwimu zinaonesha mpaka sasa asilimia 98 ya watanzania wanafahamu kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika Agosti-23 mwaka huu.
Kauli hiyo ya Waziri mkuu imetolewa leo kwa niaba yake na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye katika tamasha la Uhuru Fm Sensa Marathon lililofanyika kwenye uwanja wa Majengo Mtama mkoani Lindi.
Amesema huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo afya,elimu na huduma nyingine,zitaboreshwa zaidi iwapo serikali itakua na takwimu sahihi za wananchi wake.
Akizungumzia watu wenye mahitaji maalumu,amesema watu hao ni lazima wahesabiwe ili nao takwimu zao zipatikane,na wahudumiwe vizuri na serikali.
Naye mbunge Salma Kikwete ambaye ni mbunge wa Nchinga na mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Lindi,amesema wabunge wa mkoa huo na wananchi wao,wamejipanga kuhesabiwa Katika zoezi la sensa ya watu na makazi.
Mbunge Salma amesema zoezi Hilo mwaka huu litafanyika kisasa zaidi,tofauti na miaka iliyopita.Awali kaimu naibu mkurugenzi wa Uhuru Fm Bi. Amina.
Amina Aziz, amesema Uhuru Fm imeamua kuandaa marathon hiyo,kwa nia ya kuunga mkono juhudi za serikali katika zoezi la sensa ya watu na makazi.