…………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewashauri wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako na Watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa zilizo kwenye sekta ya Maliasili na Utalii kwa kuwa sekta hiyo chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan imejaa fursa nyingi zenye soko la dani na nje ya nchi.
Waziri Balozi Dkt.Pindi Chana ameyasema hayo leo Agosti 11, 2022 mjini Makambako mkoani Njombe wakati Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alipokua njiani kuelekea mkoani Iringa.