Afisa Mkuu wa Masoko Kampuni ya Parimatch Bi. Luby Chuku (kulia) akishika jezi ya Kablu ya Mbeya City baada kuingia makubaliano ya mkataba wa kuidhamini hiyo katika kipindi cha msimu wa mwaka 2022/2023.Afisa Habari wa Kampuni ya Parimatch Tanzania, Bw. Ismael Mohamed (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 9/8/2022 jijini Dar es Salaam kuhusu Kampuni ya Parimatch Tanzania kuingia makubaliano ya mkataba wa kuidhamini klabu ya Mbeya City katika kipindi cha msimu wa mwaka 2022/2023.
Picha na namba 3 na 4 : Uongozi wa klabu ya Mbeya City pamoja Kampuni ya Parimatch wakiwa katika picha wakati wakizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 9/8/2022 jijini Dar es Salaam.
…………………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Kampuni ya Parimatch inayofanya shughuli za michezo ya kubashiri mtandaoni imeingia makubaliano ya mkataba wa kuidhamini Klabu ya jiji la Mbeya ‘Mbeya City’ ambayo inashiriki michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika msimu wa mwaka 2022/2023.
Udhamini huo ni fedha taslimu, vifaa vya michezo pamoja na kufanya ukarabati mdogo wa uwanja wa Sokoine hasa katika eneo la kukaa benchi la ufundi, ukarabati huo utafanya kwa awamu ili kuufanya uwanja kuendelea kuwa na sifa ya kuchezewa michezo ya ligi kuu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 9/8/2022 jijini Dar es Salaam Afisa Habari wa Parimatch Tanzania, Bw. Ismael Mohamed amesema kuwa mkataba huo una faida kwa pande zote mbili katika kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Klabu ya Mbeya City inafanya vizuri.
Bw. Mohamed amesema kuwa Mbeya City ni miongoni mwa klabu kubwa hapa nchini Tanzania hususani katika kuwa na idadi kubwa mashabiki na ushawishi katika soka.
“Tumeamuna kurejea tena kufanya udhamini na Mbeya City kwa msimu huu mpya, kama mtakumbuka vizuri msimu 2020/2021 tulikwa wadhamini wakuu kwa mara ya kwanza lengo ni kuhakikisha tunaendelea kuinua sekta ya michezo” amesema Mohamed.
Amesema kuwa Parimatch jukumu lao kubwa ni kuhakikisha michezo inakua kuanzia ngazi ya chini hadi kimataifa pamoja kuwa na mafanikio makubwa.
Amefafanua kuwa wataendelea na michakato mbalimbali ya kuunga mkono vilabu vingine kutoka ligi kuu, ligi daraja la kwanza pamoja na vilabu Chipukizi jambo ambalo litasaidia kutoa ushirikiano kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi kuhakikisha ligi za Tanzania zinapiga hatua.
Kwa upande wa uongozi wa klabu ya Mbeya City wameishukuru kampuni ya Parimatch kwa kuweka udhamini katika klabu yao kwani unakwenda kuwa chachu ya kuleta mafanikio katika kuhakikisha wanafanya vizuri.
Kampuni ya Parimatch ni wadua wakubwa wa michezo ambapo wamekuwa wakidhamini klabu mbalimbali duniani ikiwemo katika Ligi kuu ya Uingereza (EPL) katika klabu ya Chelsea na Leicester City pamoja na kuendesha promotion ya bega kwa bega na mashabiki wa klabu na wapenzi wa soka.