Jamilah Ntaru Mtaalam wa bima za COMESA kutoka Shirika la Bima la Taifa NIC mkoa wa Songwe akifafanua jambo wakatialipozungumza nawaandishi wa habari kuhusu bima hizo kwenye maonesho ya Nanenane 2022 yaliyomalizika jana kwenye uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Meneja wa Shirika la Bima la Taifa NIC mkoa wa Mbeya Bw, Justine Seni akizungumzia kuhusu mawakala wa shirika hilo jinsi wanavyosaidia biashara ya shirika hilo kupanuka zaidi na kuwafikia wateja wengi zaidi.
Mhasibu wa Shirika la Bima la Taifa CPA Hilal Seif akiwaelezea jambo baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la NIC katika maonesho ya Nanenane yaliyomalizika jana kwenye uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Meneja wa Shirika la Bima la Taifa NIC mkoa wa Mbeya Bw, Justine Seni akipitia nyaraka za baadhi ya wateja waliofika katika banda la shirika hilo lili kupata huduma.
Maofisa wa Shirika la Bima la Taifa NIC wakijadili jambo katika maonesho hayo.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Yessaya Mwakifulefule kushoto akijadili jambo na baadhi ya watumishi wenzake wakiwa katika banda la shirika hilo kwenye maonesho ya Nanenane yaliyomalizika jana kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya.
………………………………………..
Shirika la Bima la Taifa (NIC) limezungumzia uwepo wa Bima ya COMMESA ijulikanayo kama (International Trade) inayohusisha magari yote yanayosafirisha mizigo kutoka Bandarini kuelekea katika nchi za jirani zilizopo katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) lengo likiwa ni kulinda vyombo vya moto ambavyo vinasafirisha mizigo kwenda nje ya Tanzania.
Akizungumza kwenye mahojiano maalum wakati wa kilele cha sikukuu ya wakulima Nanenane iliyohitimishwa rasmi Kitaifa Agosti 8,2022 katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya, Afisa wa Bima kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC) Jamila Ntaru amezungumzia umuhimu wa uwepo wa huduma hiyo ambapo amesema kuwa magari yote yanalazimika kukata Bima hiyo ili kupata kibali cha kuvuka kwenda nchi jirani.
“Hii ni Bima ambayo ipo sana katika mipaka yetu na kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda tumefungua mipaka zaidi kwa kuweka matawi yetu katika mipaka yetu yote ili iweze kuwahudumia wasafirishaji kwa haraka na ukaribu zaidi” amesema Ntaru.
Amefafanua kuwa awali Bima hiyo ilikuwa ikitolewa katika Ofisi za makao makuu zilizopo Jijini Dar es salaam pekee hali iyopelekea usumbufu kwa wasafirishaji na kuchelewa kufanya safari zao ndipo Shirikia liliona ipo tija kwa huduma hiyo kutolewa moja kwa moja katika mipaka ili kuwafanya wadau hao kupata huduma hiyo kwa haraka zaidi.
“Kule mipakani tunafanyakazi masaa 24 kwa sababu tunajua magari yetu yanayosafiri huwa yanatembea muda wote hivyo kwa kurahisisha hilo tunafanyakazi muda wote jambo ambalo limerahisisha sana kupungua kwa foleni mipani” amefafanua Ntaru.
Shirika la Bima la Taifa (NIC) liliweka kambi katika maonesho ya Kilimo Nanenane kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali kufahamu Shughuli za Bima zinazotekelezwa na la Shirika hilo.