Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiwa katika ziara mkoa wa Kilimanjaro amezungumza kwa simu na Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso kufafanua kuhusu Mradi wa Maji wa Mwanga, Same mpaka Korogwe, katika mkutano wa ndani wa Halamshauri Kuu ya Wilaya ya Same, tarehe 6 Agosti, 2022.
Ambapo Katika Mazungumzo hayo, Mhe Waziri amewaeleza wananchi kuwa Mradi huo umechelewa kukamilika kutokana na changamoto za kimkataba ambazo zimekwisha patiwa ufumbuzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hivyo, ndani ya miezi Sita Mradi huo utakuwa umekamilika na wananchi wa Mwanga – Same – Korogwe wataanza kupata maji safi, salama na yenye kutosheleza.
Hata hivyo Katibu Mkuu ameelekeza kuwa, wakati mradi huo unaendelea kutekelezwa, kwa kuwa wananchi wanakero kubwa ya maji, Wizara ichimbe visima viwili kwa ajili ya kupata maji, ambapo Mhe. Waziri amepokea maelekezo hayo, na kuahidi kutekeleza ndani ya wiki moja.
#Chongolokazini
#KaziInaendelea