………………
Na Mwamvua Mwinyi, Morogoro
MKUU wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakar Kunenge amesema Kanda ya Mashariki imedhamiria kuwa Kanda ya Mfano katika Uwekezaji mbalimbali kutokana na uwepo wa Fursa nyingi za Uwekezaji katika Sekta ya Mifugo, Uvuvi, Madini, Viwanda, Utalii, Kilimo.
Akishiriki kwenye Ufunguzi wa Maonesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki,yaliyofunguliwa na Mizengo Kayanza Peter Pinda Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Nne alimshukuru, kwa kubali kuwa Mgeni Rasmi kwenye Ufunguzi huo.
“Tumekupendeza uwe Mgeni Rasmi kwa kuwa wewe ni Mkulima Mzoefu na tunajua wakati ukitembelea mabanda hutaangalia tu bali utatoa maelekezo na mapendekezo katika kuboresha Maonesho yetu haya” Alieleza Kunenge.
Nae Pinda alisema Kanda hiyo ya Mashariki ni kanda inayokuwa kwa kasi ni kanda ya Kiuchumi.
Ameeleza kanda hiyo ina Miundombinu Muhimu ikiwemo Reli ya Mwendokasi, Barabara za Kisasa, Viwanda Vingi na Vyuo vya Elimu vyingi.
Ametaja Mikoa hiyo ya Kanda ya Mashariki ina Idadi kubwa ya wakazi zaid Milioni 13 na kusema ni Soko kubwa ambalo likitumika Vizuri litatusogeza mbele kama Nchi.
Pinda Ameeleza kuwa sekta ya Kilimo ni Muhimili muhimu kwa uchumi kwa maana ya Kilimo Mazao, Mifugo Uvuvi na Misitu.
Ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kuendelea kukuza kilimo na Mifugo kwa kuongeza Bajeti za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambapo Ameeleza mwaka 2021 kilimo kilichangia Asilimia 61 ya Ajira. “Ni muhimu kusisitiza haya ili tunapokuja kwenye Maonesho ya Nane nane tupate Maarifa, Teknolojia na ujuzi ili tunaporudi kwenye Maeneo yetu tukayatumie” Ameeleza Pinda.
Ameeleza tupime Matokeo ya Maonesho haya kwa Wanchi ikiwemo kuondokana na Utapiamlo kwenye maeneo yetu.
Ameeleza kuwa Vyuo vya Utafiti vifanye kazi kwa kuleta Serikalini tafiti ambazo zina Matokeo chanya kwa Wananchi wetu.
Ameeleza kuwa baada shughuli ya Nane nane tukahimize Kilimo na ufugaj sahihi ili ifikapo 2030 Kilimo kikue kwa Asilimia 10.