Diwani wa Kata ya Kipawa jijini Dar es salaam Aidan Kwezi akizungumzia namna kata yake imejipanga kuendelea kuhamasisha zoezi la sensa na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.
……………,….
NA MUSSA KHALID
Wananchi wa Kata ya Kipawa jijini Dar es salaam wametakiwa kuhakikisha ifikapo Agost 23 mwaka huu wanashiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi ili kuisaidia serikali iweze kufanikisha mipango ya kimaendeleo iliyoiweka.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Diwani wa Kata ya Kipawa Aidan Kwezi amesema mipango yao ni kuendelea kuwasihi wananchi kuufahamu umuhimu wa zoezi la sensa kwani litasaidia kurahisisha mipango ya kiserikali.
Aidha Diwani Kwezi amesema kuwa wanatumia njia mbalimbali katika kuwaelimisha wananchi kuhusiana na sensa ikiwemo mikutano mbalimbali,mitandao ya kijamii,vyombo vya habari na kuandaa michezo mbalimbali yenye lengo la kutoa elimu na kuhamasisha zoezi hilo la sensa.
“Kikubwa tunawaeleza umuhimu wa zoezi hili Kwa maana ndo litafanya sasa serikali iweze kupanga mipango ya kimaendeleo na mikakati mingine pindi watakapojua idadi ya watu Pamoja na Makazi”amesema Diwani Aidan
Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka Wananchi wa kata hiyo kutokuwa na Dhana potofu badala yake wajitokeze kwa wingi Kwa kufanya hivyo itasaidia kuupa urahisi serikali Pindi inapotaka kujua Takwimu za wanachi wake.
“Wananchi wetu huwa pia tunapokaa nao kwenye vikao tunawakumbusha wajibu wa kushiriki zoezi Hili la sensa kwani ni muhimu Kwenye maendeleo”ameendelea kusisitiza Diwani Aidan
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Kata ya Kipawa wameeleza umuhimu wa sensa huku wakiwataka hasa vijana kuhakikisha wanashiriki katika zoezi hilo kwa litasaidia serikali kujua takwimu ya kwa wananchi wake.
Katika Hatua Nyingine Diwani Kwezi amesema wameamua pia kuanzisha Mashindano ya Aidani Kwezi Diwani Cup lengo likiwa ni kuhakikisha vijana wanajipatia ajira lakini kuwahamasisha namna ya kujishighulishq katika Matukio mbalimbali ya kijamii likiwemo sensa.
Sensa ya watu na makazi inatarajiwa kufanyika Agost 23 mwaka huu hivyo watanzania wameendelea kukumbushwa kushiriki katika zoezi hilo ili liweze kukamilika kama serikali ilivyopanga.