Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akiwasalimia akina mama waliofika kumpokea katika kata ya Masama Rundugai Chekimaji Hai mara baada ya kuwasili kukagua ujenzi wa kituo Cha Afya na nyumba za watumishi kijijini hapo Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Katika ujenzi wa Kituo hicho wananchi wamechangia jumla ya shilingi milioni 11 na Halmashauri ikichangia shilingi milioni 28 na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa shilingi Milioni 500.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akivishwa skafu na vijana wa Chipukizi mara baada ya kuwasili wilayani Hai kwa ziara ya kukagua, kuhamasisha na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025, Katika ziara hiyo Katibu Mkuu ameongozana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipewa heshima za kimila na Mzee Kimanyi Pankiapo Laiza mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya na ujenzi wa nyumba za watumishi Chekimaji kata ya Masama Rundugai wilayani Hai, Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na wakinamama wa Rundugai, Hai mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Hai Sahasisha Mafue mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Chekimaji Rundugai, Hai mkoani Kilimanjaro
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisikiliza taarifa ya ujenzi wa mradi wa Kituo cha Afya na Nyumba za Watumishi kutoka kwa Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Wilaya ya Hai Dkt.Itikija E. Msuya(kushoto).
Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya na ujenzi wa nyumba za watumishi Rundugai, Hai mkoani Kilimanjaro.