…………………….
Na. Damian Kunambi, Njombe
Katika kuhakikisha kuwa taifa la Tanzania linaendelea kuwa na amani na Rais wake anakuwa na afya bora viongozi mbalimbali wa serikali, kidini na kimila mkoani Njombe wameungana na kufanya kongamano la kuliombea taifa hilo na Rais Samia Suluhu Hassan.
Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Wazi Kindamba ambaye siku chache zilizopita amepangiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Songwe ambapo lengo la kongamano hilo ikiwa ni kuliombea taifa pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan.
Kindamba amesema kuna kila sababu ya kufanya maombi hayo kwakuwa Rais Samia amefanya maendeleo makubwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo mkoa wa Njombe ambapo wameweza kupokea fedha zaidi za miradi ya barabara, vituo vya afya, maji, shule na sekta nyinginezo.
Aidha Kindamba ametumia kongamano hilo kuwaaga wana Njombe huku akimshukuru Rais kwa kuendelea kumwamini na kumpangia mkoa mwinine ambao ni mkoa wa Songwe.
Wabunge wa mkoa wa Njombe nao ni moja ya viongozi waliohudhulia kongamano hilo akiwemo waziri wa Maliasili na utalii Balozi Dkt. Pindi chana ambaye amesema Rais Samia amefanya makubwa kupitia The Royal Tour ambapo kwa sasa watalii wamekuwa wakimiminika katika maeneo mbalimbali ya vivutio vyetu.
Naye Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema vijana ni kundi mojawapo lenye nguvu na linaloweza kudumisha amani hivyo ameipongeza serikali kwa kuanza kutoa ajira mbalimbali kwa vijana huku akiiomba serikali kuendelea kuwaangalia zaidi vijana hao.”
Kuna moja ya watumishi wa Mungu amezungumza vizuri sana juu ya vijana, kiukweli nimeguswa na kundi hili hivyo tunaiomba serikali izidi kuwaangalia ili amani yetu izidi kudumu”, Amesema Kamonga.