Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi Mindi Kasiga Mkurugenzi wa Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Jne na Ushirikiano wa Kimataifa wakati alipowasili kwenye Chuo Cha Diplomasia Kurasini Jijini Dar es Salaam kufungua mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za Diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa yanafofanyika kwa siki mbili kuanzia leo Julai 27,2022 na 28, 2022.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi Mstaafu Patrick Tsere wakati alipowasili kwenye Chuo Cha Diplomasia Kurasini Jijini Dar es Salaam kufungua mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za Diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa yanafofanyika kwa siki mbili kuanzia leo Julai 27,2022 na 28, 2022. katikati ni Balozi Mindi Kasiga Mkurugenzi wa Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula aki na viongozi mbalimbali wakati apowasili Chuo Cha Diplomasia Kurasini Jijini Dar es Salaam kufungua mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za Diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa yanafofanyika kwa siki mbili kuanzia leo Julai 27,2022 na 28, 2022
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika semina ya waandishi wa habari Chuo Cha Diplomasia Kurasini Jijini Dar es Salaam wakati akufungua mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za Diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa yanafofanyika kwa siki mbili kuanzia leo Julai 27,2022 na 28, 2022
Bw. Justine Kisoka Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango ya Nje akiwasilisha mada katika semina hiyo.
Balozi Mstaafu Peter Kallaghe akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za Diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa yanafofanyika kwa siki mbili kuanzia leo Julai 27,2022 na 28, 2022.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.
Balozi Mindi Kasiga Mkurugenzi wa Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa akifafanua jambo katika mafunzo hayo.
Picha pamoja.
………………………….
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amefungua mafunzo ya uandishi wa habari za kidiplomasia kwa waandishi wa habari nchini.
Akifungua mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika katika Chuo cha Diplomasia jijini Dar es Salaam, Balozi Mulamula amewataka watendaji wa Wizara kuhakikisha wanaimarisha mahusiano kati ya wizara na vyombo vya habari.
‘Tuwe pamoja siku zote tuendelee kushirikiana, vyombo vya habari ni wadau muhimu, tufanye kazi pamoja kwa manufaa ya nchi yetu,’ alisema.
Amesema waandishi wa habari wanajukumu la kuilinda na kuitetea taswira ya Tanzania kupitia kazi zao na kuwataka waandishi wa habari nchini kuzingatia taswira ya nchi wakati wanatekeleza majukumu yao.
“Wanahabari, tuko hapa kuelimishana juu ya kuandika habari za kidiplomasia, niwaombe kwanza mhakikishe mnailinda taswira ya nchi, hii ni nchi yetu wote, ikiharibika taswira yake hata wewe uliyeandika pia utakutana na athari zake, hata uende wapi utajulikana kama Mtanzania. Mnapoandika mzingatie uzalendo na miiko ya taaluma ya uandishi wa habari,” alisema Balozi Mulamula.
Pia aliongeza kusema mafunzo haya ambayo yatakuwa endelevu yanalenga pamoja na mambo mengine kutoa uelewa kuhusu masuala ya diplomasia ikiwemo Itifaki, Diplomasia ya Umma, Uzalendo na Mawasiliano ya kimkakati baina ya Tanzania na nchi zingine.
Kadhalika, aliwashukuru waandishi wa habari kote nchini kwa ushirikiano uliopo kati yao na wizara na kuwataka kuzingatia mafunzo yatakayotolewa kwao.
“Nawashukuru kwa ushirikiano na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa Wizara na Sera ya Mambo ya Nje inayosisitiza katika Diplomasia ya Uchumi. Nawaomba mzingatie mafunzo haya kwani yatakuwa na tija kubwa kwenu,” alisisitiza Balozi Mulamula.
Awali akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Serikali Waziri ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga alieleza kuwa mafunzo hayo yameandaliwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini katika eneo la kuandika habari za kidiplomasia.
Amesema mafunzo hayo yatakuwa endelevu kwani kufanya hivyo kutasaidia kuboresha uandishi na kuwa daraja kati ya Wizara na waandishi wa habari na hivyo kuwafikia wananchi wengi.
Mafunzo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yamewashirikisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya hapa nchini.