lMakamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo Julai 26,2022 alipokuwa akizungumza na wana CCM na wananchi mjini Sumbawanga baada ya kupokelewa katika ofisi za Chama mkoani Rukwa
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wasijisahau katika kuwatumikia wananchi na kuwatatulia kero zao.
Kinana ameyasema hayo leo Julai 26,2022 alipokuwa akizungumza na wana CCM na wananchi mjini Sumbawanga baada ya kupokelewa katika ofisi za Chama mkoani Rukwa kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuimarisha uhai wa Chama,
“Wananchi wanawachagua viongozi ili wananchi wasikilizwe na viongozi, kazi ya viongozi ni kuwasikiliza wananchi, kazi ya viongozi kusikiliza matatizo ya wananchi, kazi ya viongozi ni kusikiliza kero za Watanzania wananchi, ndio waliowaajiri.
“Wakati mwingine viongozi tunajisahau tukishapata uongozi, tunawasahau waliotupa uongozi, wananchi, lazima mzungumze nao, mfanye vikao na wananchi muulize shida zao.” Amesema.
Aidha, Kinana amewakumbusha viongozi kuwa jukumu lao la msingi ni kuwatumikia wananchi na kuhakikisha wanawatatulia shida zao ili hatimaye wajiimarishe kimaisha.