Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Joseph Mkirikiti wakati alipowasilia mkoani Rukwa na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali katika Kata ya Paramawe wilayani Nkasi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoani Rukwa wakati lipowasilia mkoani humo na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali katika Kata ya Paramawe wilayani Nkasi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana akisalimian Mubnge wa Sumbawanga Aishi Hillaly alipowasilia mkoani Rukwa na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali katika Kata ya Paramawe wilayani Nkasi.
Picha mbalimbali zikionesha wana CCM na wananchi waliojitokeza kumlaki Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Na Mwandishi Wetu Rukwa
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewasilia mkoani Rukwa na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali katika Kata ya Paramawe wilayani Nkasi.
Akizungumza katika mapokezi hayo, Kinana ambaye ameambata Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema anaridhishwa na namna wananchi wa Rukwa wanavyojituma katika kutekeleza shughuli za kiuchumi.
“Nataka kuwapongeza ndugu wananchi kwa kutupokea vizuri, tunawapenda, tunawaheshimu. Najua mnajituma, kazi ya Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata maendeleo anayostahili…kila siku tunazungumza juu ya sekta binafsi, sekta binafsi inaanza na mwananchi wa kawaida anayejituma, anayehangaika, anayefanya biashara yake ili kila siku mfuko wake uendelee kunona apate fedha nyingi zaidi.
“Kazi ya Serikali ni kutatua matatizo kwa wananchi, kurahisisha shughuli zao za kibiashara ili waweze kufanikiwa. Niko mkoani kushauriana na viongozi wenzangu ili tuweze kuwasaidia wananchi wapige hatua.
” Nawashukuru sana kwa mapokezi na nawatakia kila la heri wale tunaoangana na bila shaka tutafanya kazi pamoja wale wanaotupokea na wananchi nawatakia kila la heri na bwana awe nanyi,” amesema Kinana akipoewa Rukwa akitolea Mkoa Katavi alikofanya ziara kwa siku mbili.
Akiwa mkoani Rukwa Kinana atatembelea miradi mbalimbali kukuta na kuzungumza na viongozi na wananchi.