Mkurugenzi wa Taasisi ya ASEDEVA Isack Abeneko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam akieleza kuhusu Tamasha la Kimataifa la Dansi la Haba na Haba 2022 litakalofanyika July 29-30 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Achiles Bufure amesema dhamira Museam Arts Explosin –(MAE) akiwaeleza wanahabari dhamira ya kufanyika tamasha hilo.
Meneja Mradi wa – ASEDEVA Upendo Manase akiwaeleza wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu Tamasha la Kimataifa la Dansi la Haba na Haba 2022 litakalofanyika July 29-30 mwaka huu.(picha na Mussa Khalid)
………………………..
NA MUSSA KHALID
Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Sanaa kwa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi Katika Afrika (ASEDEVA) wamewataka vijana wanaofanya sanaa ya muziki kuzingiia tamaduni za asili ili kuendelea kuutangaza urithi wa nchi.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati akitambulisha Tamasha la Kimataifa la Dansi la Haba na Haba 2022 litakalofanyika July 29-30 mwaka huu,Mkurugenzi wa Taasisi ya ASEDEVA Isack Abeneko amesema lengo lao ni kuhakikisha wanawasaidia vijana kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia sanaa zao.
Abeneko amesema taswira ya tamasha hilo ni kuwawezesha wasanii kupata mbinu mpya ambazo zinaweza zikawasaidia vijana hao kuboresha kazi zao za sanaa ili ziweze kuwa na ueledi.
‘Wiki hii kuanzia leo Tar 25 -30 tutakuwa na tamasha ambalo linaitwa Haba na Haba Internationa Dance Festival ambalo tumeanza na warsha na zipo za aina tano zikiwemo za ngoma za Asili kwa ajili ya kuwafundisha vijana wanaofanya miondoko ya kisasa kuzingatia tamaduni za asili asilia,kufaragua wasanii watakuwa wanafundishwa,masai dansi pia itakuwepo’amesema Abeneko
Amesema tamasha hilo litafanywa na wasanii tofauti tofauti akiwemo Fenando Anuang’a kutoka Ufaransa,Duduzile Voigts kutoka Ujerumani,Luanda Mori kutoka Swizland,Safi Theather kikundi cha asili cha nyumbani na Thami Mjela kutoka Afrika ya Kusini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Achiles Bufure amesema dhamira Museam Arts Explosin –(MAE) ambalo linafanyika kila mwisho wa wezi ni kuwasaidia vijana wa kitanzania wanaofanya sanaa kutangaza kazi zao.
‘Sisi kama Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni kama kawaida tumekuwa tukitoa nafasi kila mwisho wa mwezi kupitia program ya MAE ili wasanii wa kitanzania waweze kuonyesha kazi zao hivyo ASEDEVA wamepata nafasi hiyo kufanya kazi zao za kisanii’amesema Bufure
Upendo Manase ni Meneja Mradi wa – ASEDEVA na Tamasha la Kimataifa la Dansi la Haba na Haba 2022 amesema tamasha hilo ni la sita tangu kuanzishwa ambapo wamekuwa wakihusisha sanaa ya ngoma za asili na masuala ya ubunifu.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika July 29 na 30 mwaka huu hivyo wananchi wametakiwa kutumia fursa hiyo katika kujitokeza kwa wingi ili kutangaza kazi ziweze kutambulika kitaifa na kimataifa.