………………….
Adeladius Makwega-DODOMA”…Tatizo la wananchi wa Tanzania ni uchumi, tatizo la wananchi wa Tanzania ni ajira, umasikini unaondolewa na uchumi bora, uchumi imara.
Ajira zina-zinapatikana kwa wingi wakati uhumi ni viabrant umechangamka kabisa. Rais Mkapa alitufanyia kazi nzuri sana alitutoa katika ukuaji wa uchumi chini-chini huko asilimia 3-4 na wakati anamkadhi Rais Kikwete uchumi ulikuwa kwa asilimia 7.
Tanzania ilikuwa inasifika kwa sababu tumetoka mbali hadi kufikia asilimia 7 ile miaka 10 ya Rais Mkapa…”Hiyo ni hutuba ya mwanasiasa wa Tanzania ya miaka karibu saba iliyopita.“…Rais Kikwete amepokea madaraka uchumi unakua kwa asilimia 7, 2015 uchumi ulikuwa unakua kwa asilimia karibu na 7 wameandika sasa hivi kwenye gazeti, maana yake miaka10 tumepiga mark time, tumebaki palepale, tatizo la kubaki palepale maana yake tumerudi nyuma kwa sababu mwaka 2005 wakati uchumi unakua kwa asilimia 7 idadi ya watu ilikuwa ngapi? Je leo miaka kumi baadaye idadi ya watu imeongezeka kiasi gani ? Nyie mnajua hesabu,watu wameongezeka zaidi ya milioni 10.
Sasa midomo imeongezeka, miguu imeongeza lakini ukuaji upo pale pale. Sasa ni jambo la ajabu bei ya kilo moja sukari ni ya kuruka Ndugu Mkapa aliiacha kilo shilingi 600/700/- sasa shlingi ngapi mnanunua ? Shilingi 2000/- na wakati mwingine inakuwa zaidi, midomo imeongeza bidhaa kudu…
”Kwa sasa msomaji(2022) sijajaliwa kufahamu uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia ngapi? Lakini bei ya kilo moja ya sukari ni shilingi 2800.“…Hili kuwaondoa watu kwenye umasikini, wataalamu wote wa Ulaya , Marekani, Uchina wanasema ukuaji wa uchumi wa nchi lazima ufikie angalau asilimia 10.
Kutoka 7 hadi 10 si mbali…tunapenda sana kuzungumza habari za Wachina… Wachina… lakini hatuwajui, wanaongozaje nchi?Wanamikakati gani?
Wachina wamekuwa wakiukuza uchumi wao mpaka asilimia 15 na zaidi, na mimi najua baadhi ya mikoa ya China ilikuwa inakuza uchumi wake mpaka asilimia 30. Sisi hapa kwa hali yetu kama watu wanakuwa wanyenyekevu kupata mawazo ya wenzao hapa tunaweza kukuza uchumi wetu ndani ya miaka 5 tukafika asilimia 10 na miaka 5 tukafika mpaka asilimia 15.”Mwanasiasa huyu mkongwe tangu TANU na hadi CCM aliamua kuongea,“Chukulia mfano mkulima anayelima mahindi heka moja anapata magunia 5 ukimfundisha kilimo bora atatoka kuvuna magunia 5 hadi magunia10i, huo utakua ukuaji wa 100%.
Je akifika magunia 20 (200%). Chini ya Mwalimu Nyerere kule mikoa ya Nyanda za Juu Kusini sisi tulifanya hivyo na mimi nilikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, miaka ya 70, tulifanya kazi ya kuwafundisha wananchi kilimo bora cha mahindi Ruvuma, Iringa, Mbeya na Rukwa tulikwenda hadi vijiji tunafanya mikutano ya Kilimo Bora, wale si ndiyo wanatulisha nchni nzima? Ziada kubwa ya mahindi kwa sehemu kubwa inatoka kule, kwanini ? Kwa sababu walipewa maarifa,Tulifanya kazi…
”Siku ya leo nimeamua kukupa hii tafakari ya Kingunge Ngombale Mwiru kwa kwa sababu ngingi sana.Kwa kifupi kwangu ninapokaa Chamwino Ikulu mwaka wa kilimo 2021/2022 nililima robo tatu ya heka na nikapata magunia sita ya mahindi huku majirani zangu wengi hawakuambulia kitu, kilichonisaidia ni matumizi ya mbegu bora za mahindi kwa maana nilinunua mifuko miwili mbegu bora kwa shilingi 22,000/- Huku gharama ya kupalilia eneo hilo haikufika hata shilingi 60,000/-kwa palizi mbili.
Mahindi yangu yaliweza kustahimili mvua kidogo na wale majirani waliopanda mbegu za asili mahindi yao yalirefuka tu na mwisho wa siku waliambulia patupu mahindi yaoa machache mno yalibeba na mwisho wa siku kukauka kwa kukosa mvua.Shida kubwa ni uwezo wa kupata mbegu bora ambacho hicho ni sehemu ya kilimo bora.
Kuna wakati niliwahi kwenda Arusha-Tanzania nilikutana na kijana mmoja aliyemaliza Chuo KIkuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kijana huyu alipata kazi katika kampuni moja ya uzalishaji wa mbegu bora ya Wamerakani, alifanya kazi hapo kwa mwaka akiwa msimamizi wa mradi huo.
Taasisi hili iliamua kumuhamshia Mwanza, kijana huyu wa Kiarusha hakulidhishwa na uhamisho huo kwakuwa Arusha ni kwao tangu enzi kama alikuwa akitoka Arusha ni masomo tu.
Kijana huyu akaamua kuacha kazi. Kampuni ile ya Wamarekani ikamua kumuongeza mshahara kutoka Milioni 1.5 hadi milioni 3 aende Mwanza kijana aligoma. Kuogezwa mshahara huko kulimsitua mno na kufahamu ujuzi wake ulivyokuwa mkubwa na mahitaji ya kampuni hii kwake.Uhamisho huo ulimtoa usingizi kijana huyu wa Kitanzania akajiuliza,
“Kwanini nisianzishe kitalu changu cha kuzalisha mbegu kwa kutumia elimu yangu ya SUA na uzoefu nilioupata kutoka Kampuni hii ya Kimarekani?”Kijana wa Kiarusha akakata shauri na kuamua kuanzisha kitalu chake nayo jamaa wa Kimarekani wakamwambia basi abaki Arusha na wanamuongezea mshahara kutoka milioni 3 hadi 4 mwanakwetu.
Kijana wa Kiarusha aligoma na akaacha kazi na kuanzisha mradi wake wa kuzalisha mbegu. kijana huyu alichukua mishahara yake na fedha zake kidogo na kule kuaminiwa kwake na baadhi watu aliofahamiana nayo akiwa mtumishi wa kampuni ya Kimarekani na kuanza uzalishaji huo wa mbegu bora.
Hivi ninavyozungumza kijana huyu ambaye alinipatie mbegu ya pensheni niliyootesha nyumbani kwnagu ameweza kufungua matawi kadhaa ya kuzalisha mbegu bora Arusha, Mwanza na Singida.
“Sasa sijaiona faida kubwa kwa kuwa fedha zangu karibu nyingi nimeziingiza kufungua matawi ya Mwanza na Singida huku nikifamya vizuri sana ninaimani nitafika mbali.”Jamani serikali ushauri wangu hawa wanafunzi wanohitimu SUA na vyuo vingine vya kilimo wakishahitimu waambieni warudi katika mikoa yao wapeni mitaji kwa mkopo kama ule mkopo wa elimu ya juu.
Dhamani yao iwe cheti cha Stashahada, Shahada, Shahada ya Uzamili na hata Shahada ya Uzamivu katika kilimo wafungie miradi ya kuzalisha Mbegu bora na kilimo bora na kila Halmashauri iwanunulie wakulima wake ambao hawana uwezo mbegu bora kama wale majirani zangu ili wazipande waongeze kipato.Kwa hakika kila mwananchi mwenye uhitaji akipatiwa mbegu bora bure mwaka wa kwanza akivuna akiuza mazao yake mwaka wa pili mbegu hatopewa bure bali atanunua mwenyewe kwa kuwa atakuwa na uwezo hapo wakulima wetu watafikisha tija ya 200% ya Kingunge Gombale Mwiru na Tanzania tutakqquwa na ule unyenyekevu wa kufanyia kazi mawazo ya