Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Mary Masanja akisalimiana na Chifu wa Kabila la Wasafwa Mbeya Mjini Roketi Masoko Mwashinga alipowasili katika Tamasha la utamaduni wa Mtanzania Mwaka 2022 kwa watu wa Jamii ya wasafwa linalofanyika kwa siku tatu July,22 -24 mwaka huu katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Mary Masanja akikata utepe kufungua nyumba za watu wa Jamii ya wasafwa kutoka katika Mkoa wa Mbeya katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam.
Chifu wa Kabila la Wasafwa Mbeya Mjini Roketi Masoko Mwashinga akizungumza na waandishi wa habari kueleza namna kabila hilo linavyoendeleza utamaduni wa mtanzania.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Tanzania Dkt Oswald Masebo akizungumza na wanahabari kueleza dhamira ya Makumbusho kuendelea kufanya matamasha ya utamaduni mara kwa mara.
Chifu wa Kabila la Wasafwa Mbeya Mjini Roketi Masoko Mwashinga akimkabidhi zawadi ya chungu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Mary Masanja katika Tamasha la utamaduni wa Mtanzania Mwaka 2022 kwa watu wa Jamii ya wasafwa linalofanyika kwa siku tatu July,22 -24 mwaka huu katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Mary Masanja akicheza ngoma ya utamaduni ya Jamii ya wasafwa (picha na Mussa Khalid)
………………………..
NA MUSSA KHALID
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Mary Masanja amewataka watanzania kuupenda na kuuthamini utamaduni wao ili kuweza kuvirisisha vizazi vya sasa na baadae viepukane na kuiga tamaduni za Nje.
Naibu Waziri Masanja amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akifungua Tamasha la utamaduni wa Mtanzania Mwaka 2022 kwa watu wa Jamii ya wasafwa kutoka katika Mkoa wa Mbeya linalofanyika kwa siku tatu July,22 -24 mwaka huu katika kijiji cha Makumbusho.
Aidha Masanja amesema lengo la serikali ni kuendelea kuhamasisha utalii wa utamaduni nchini ili kuionyesha jamii uhalisia wa mtanzania na makabila yao.
‘Mwaka jana tulikuwa na utalii wa Wakinga tuliadhimisha na mwaka huu tumekuwa na utamaduni wa Wasafwa hivyo kwenye eneo hili la utamaduni tunajaribu kuionyesha jamii kuhusu tamaduni za mtanzania ili kuziendeleza mila na desturi zetu kwani ndizo zimetufanya watanzania kuwa na amani na utulivu’amesema Naibu Waziri Masanja
Amewakumbusha Watanzania kufahamu kuwa Kijiji cha Makumbusho kinaendelea kuboresha utamaduni wa Mtanzania kwa kusheheni makabila tofauti hivyo ameeleza kuwa mwezi wa tisa mwaka huu pia nwanatarajia pia kabila la wamasai watakwenda kuonyesha tamaduni zao.
Awali akizungumza Chifu wa Kabila la Wasafwa Mbeya Mjini Roketi Masoko Mwashinga amesema kabila hilo limekuwa likiendeleza utamaduni wao na amewataka vijana nchini kukumbuka walipotoka na kutizama wanapokwenda kwa kutou acha utamaduni wa kwao.
‘Kwa kweli haya ni makosa vijana wetu kumbuka ulipotoka tizama unapokwenda sasa hivi wanasema teknolojia inakuja kwa kasi lakini naomba muhiharibu utamaduni wenu’amesema Chifu Roketi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Tanzania Dkt Oswald Masebo ameipongeza jamii hiyo ya wasafwa kwa kudumisha utamaduni hivyo amewashauri watanzania kuendelea kushirikiana na Makumbusho katika kuonyesha tamaduni zao.
Amesema sababu ya umuhimu wa tamasha la utamaduni ni fahari ya Taifa la Tanzania kwani pia yanatoa nafasi ya fursa muhimu ya kubadilisha utamaduni na historia kuwa zao muhimu la utalii kutokana na sasa kuwa chanzo kikubwa cha mapato.
Hata hivyo jamii imetakiwa kujiwekea mazoea ya kutembelea na kufanya Utalii katika Makumbusho mbalimbali nchini mara kwa mara kwani watajifunza tamaduni za jamii za mtanzania zilizopo hapa Nchini.