Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akisaini kitau cha wageni katika moja ya banda la chuo kikuu cha Mzumbe,wakati akiendelea kutembelea Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo Julai 21,2022 mkoani Dar es Salaam.Pichani kati ni Katibu Mtendaji wa TCU Prof Charles Kihampa na kushoto ni Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Bi. Rose Joseph. PICHA HII IMEPIGWA NA MICHUZI JR.
watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbewakiendelea na majukumu yao ya kufanya udahili wa Papo kwa hapo kwenye Maonesho hayo.
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Bi. Rose Joseph akiendelea na majukumu yake.
PICHA NA:HUGHES DUGILO
Na: Hughes Dugilo, DAR.
Katika kuhakikisha kunakuwepo na wigo mpana kwa wanafunzi wa shahada mbalimbali zinazotolewa katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo hicho kimeanzisha Programu mpya tano zitakazoanza kutolewa rasmi katika mwaka wa masomo wa 2022/2023 katika ngazi za shahada tofauti.
Bi. Rose Joseph ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Chuo hicho amesema kuwa Programu hizo ni mpya kabisa ambazo zitatolewa kuanzia Shahada za awali hadi uzamivu.
Rose ameyasema hayo Julai 21,2022 katika mahojiano maalum na waandishi wa habari katika Maonesho ya 17 vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam ambapo mapoja na Mambo mengine Chuo hicho kinafanya Udahili wa papo kwa hapo ndani ya Banda lao.
Amezitaja kozi hizo kuwa ni pamoja na Diploma in Local Government management (DLGM), Bachelor of Public Administration in Youth Development and Leadership, Bachelor of Health Systems in Monitoring and Evaluation, Masters of Public Administration in Ethics and Governance, and PhD in Public Administration (Course Work and Dissertation).
“Hizi Kozi ni mpya kabisa hatukuwanazo mwaka jana na zinatolewa kuanzia ngazi ya Diploma hadi PhD na Kozi hizi tano tumezileta hapa kuwahamasisha wananchi wazitambue, wazijue ili waweze kupata uelewa zaidi na kuweza kuzichangamkia ili wakijiunga katika mwaka mpya wa masomowaweze kuzichukuwa” amesema Rose.
Na kuongeza kuwa “kwenye Maonesho haya kumekuwa na muamko mkubwa sana, watu wengi wanakuja hapa na kupata maelezo mbalimbali ya Kozi zetu na wengi wanajiandikisha hapahapa na kujiunga na Chuo chetu, wengi wanavutiwa na Chuo chetu kutokana na Ubora wa elimu inayotolewa, hivyo tunazidi kuwakaribisha kufika katika Banda letu”ameongeza.