Afisa Mawasiliano Mkuu kutoka Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Idara ya Usimamizi wa Maadili Rocky Setembo akitoa mada leo kuhusu misingi na kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma kwenye mafunzo elekezi kwa Mahakimu na Wasaidizi wa Kumbukumbu yanayoendelea katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Waaajiriwa wapya wa Mahakama ya Tanzania wakisiliza mada kuhusu misingi na kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma kwenye mafunzo elekezi kwa Mahakimu na Wasaidizi wa Kumbukumbu yanayoendelea leo katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.Afisa Mawasiliano Mkuu kutoka Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Idara ya Usimamizi wa Maadili Rocky Setembo akitoa bango linaloonyesha mavazi yasiyoruhusiwa na yanayoruhusiwa kwa watumishi wa umma leo wakati akitoa mada kuhusu misingi na kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma kwenye mafunzo elekezi kwa Mahakimu na Wasaidizi wa Kumbukumbu yanayoendelea katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Picha na Tiganya Vincent-JOT
………………….
Na Tiganya Vincent-Mahakama ya Tanzania-Lushoto
Waajiriwa wapya wa Mahakama ya Tanzania wameaswa kuepuka matumizi ya mitandaa ya kijamii kutuma taarifa mbalimbali za uendeshaji wa shughuli za kiutumishi kwa kuwa bado njia hiyo sio rasmi na haijaidhinishwa.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Lushoto na Afisa Mawasiliano Mkuu kutoka Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Idara ya Usimamizi wa Maadili Rocky Setembo akitoa mada kuhusu misingi na kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma kwenye mafunzo elekezi kwa Mahakimu na Wasaidizi wa Kumbukumbu yanayoendelea katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Amesema hadi sasa hakuna Waraka ambao umetolewa wa kuruhusu mitandao kama vile WhatsApp , Instragrum na twiter kutumika katika utumaji wa nyaraka muhimu za Serikali kama vile barua , waraka na madokezo.
Setembo ameongeza hadi sasa njia ambayo watumishi wa umma wanapaswa kutumia barua za kiutumishi ni kupitia Posta na barua pepe ya Serikali ambayo ina jina la Taasisi husika na kuendele ikiwa na maneno ya @go.tz na sio kwa kutumia barua pepe nyingine ambayo wamiliki wa chombo cha kutunzia kumbukumbu(Server) wako nje ya Tanzania.
Amesema matumia ya barua pepe ambazo chombo cha kutunza kumbukumbu(Server) kiko haziruhusiwi kutumika kutumia nyaraka za kiutumishi.
Aidha Setembo amewataka watumishi hao wapya kutumia muda wa Serikali kwa ajili ya kutoa huduma nzuri kwa wananchi badala ya kusoma na kujibu ujumbe katika makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii ambayo hayana tija kwa umma.
“Utakuta mtumishi mmoja wa umma amejiunga na makundi ya Whatsapp ,twiter mbalimbali kama mfano anaweza kuwa na kundi la aliosoma nao Sekondari, chuoni na kazi na makundi yote anataka kujibu kila ujumbe unaoandikwa katika kundi hali hiyo wakati mwingine inasababisha kutumia muda wa Serikali jambo ambalo ni makosa”amesema
Katika hatua nyingine Afisa Mawasiliano huyo Mkuu amewataka Watumishi hao watakapokuwa katika vituo vyao vya kazi kutumia lugha nzuri na yenye staha wanapotoa huduma kwa wateja wa ndani na wa nje ili kuepuka kuwaathiri na kuchafua jina la taasisi ambayo watakuwa wakiitumikia.