Wakii wa kujitegemea na Makamu Mwenyekiti wa MISA – TAN James Malenga akitoa mada kwa waaandishi wa habari za Mtandaoni kuhusu Sheria za Mtandaoni na sheria ya Huduma za habari katika semina yasiku moja iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) iliyofanyika leo Julai 20,2022 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Bw. Deodatus Balile akifafanua jambo katika semina ya Sheria ya Huduma za Habari 2019 iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ili kuwapa uelewa kuhusu sheria hiyo ambayo imefanyika kwenye hoteli ya Sapphire jijini Dar es salaam Leo Julai 20, 2022.
Baadhi ya waandishi wa habari za mtandao wakiwa katika semina ya Sheria ya huduma za habari 2019 iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na kufanyika kwenye hoteli ya Sapphire Leo Julai 20, 2022 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari za mtandao wakiwa katika semina ya Sheria ya huduma za habari 2019 iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na kufanyika kwenye hoteli ya Sapphire Leo Julai 20, 2022 jijini Dar es Salaam.
Kimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Anitha Mendoza akifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Wakili James Malenga kwenye Semina hiyo.
………………………………..
Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni ya mwaka 2019, inaweza kumtia mtu hatiani na hatimaye kumfunga hata kama hakufika mahakamani ili kusikilizwa imeelezwa leo Julai 20,2022.
Mtu anaweza kushtakiwa na kupelekwa mahakamani bila yeye kuwepo na akahukumiwa na kufungwa alafu ndio akatafutwa na kukamatwa kisha kupelekwa gerezani bila kujua kesi yake ilipelekwa mahakani lini, na kwa kosa gani. Ndio maana sheria hii inatakiwa kupitiwa upya.
Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA–TAN) Wakili msomi wa kujitegemea James Marenga, katika semina ya siku moja ya waandishi wa Habari za mtandanoni iliyofanyika katika Hoteli ya Sapphire Jijini Dar es Salaam.
“Sheria hii katika Kifungu cha 50(2)(b) kinaondoa haki ya mtu kukata rufaa kinyume na Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, lakini pia Kifungu cha 38(2)(b) cha sheria hii kinaruhusu usikilizwaji wa shauri mahakamani hata bila muhusika kuwepo,”. Amesema Marenga.
Hii inaweza kumnyima mtu haki ya kusikilizwa na kujieleza kwa sababu kesi itaendeshwa mahakamani hapo akiwa hayupo maana yake hataweza kujitetea au kujieleza jambo ambalo linazuia haki ya mtu kijieleza na kusikilizwa.
Wakili Marenga amesema, kwenye sheria hiyo kuna adhabu zilizowekwa kwa makosa ambayo hayapo wazi kinyume na Ibara ya 13 (6)(C) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo ni wajibu wa wadau mbalimbali kutoa maoni yao kuhusu sheria hiyo ili ifanyiwe marekebisho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Deodatus Balile amewataka waandishi wa habari za mtandao kushiriki kikamilifu. katika kutoa maoni yao kuhusu sheria ya Huduma za habari ya mwaka 2019 ili kuhakikisha inarekebishwe.