Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa katika mkutano wa kamati ya Mawaziri wanaoshughulika na udhibiti wa maafa kwa nchi wanachama wa SADC uliofanyika Lilongwe Malawi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawenea katika picha ya pamoja na Bwn. Fredrick Chiwanga (kulia) na Bwn. Lwema Taguaba katika mkutano wa kamati ya Mawaziri wanaoshughulika na udhibiti wa maafa kwa nchi wanachama wa SADC uliofanyika Lilongwe Malawi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya waziri Mkuu Meja Jerali Michaeli .M. Mumanga (kushoto) aliyeongoza ujumbe wa Tanzania.
……………….
Na Mwandishi wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameishauri sekretarieti ya SADC kwa Kushiriiana katika kuimarisha utendaji wa kazi wa Kituo cha udhibiti wa Maafa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu katika Mkutano wa kamati ya Mawaziri wanaoshughulika na udhibiti wa maafa kwa Nchi wanachama wa SADC uliofanyika Lilongwe Nchini Malawi.
Katika kikao hicho waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu aliaambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya waziri Mkuu Meja Jenerali Michaeli .M. Mumanga aliyeongeoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao hicho.