Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbalo akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa RITA jijini Dar es Salaam leo kuhusu kutoa mjadala wa Mapungufu yaliyopo kwenye katiba iliyopo na Serikali kuweka wigo mpana kwa Asasi za kiraia kujadili ili kuirebisha na kupata Katiba Nzuri.
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbalo akionesha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa RITA jijini Dar es Salaam leo kuhusu serikali kuruhusu mjadala wa Mapungufu yaliyopo kwenye katiba iliyopo na Serikali kuweka wigo mpana kwa Asasi za kiraia kujadili ili kuirebisha na kupata Katiba Nzuri.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Sheria na Katiba Dk. Damas Ndumbaro alipokuwa akizungumza nao leo jijini Dar Es Salaam.
…………………………………..
Serikali imesema itaendelea kufanyia Marekebisho mapungufu ya Katiba iliyopo na kusisitiza kuwa katiba iliyopo ni nzuri .
Akizungumza na waandishi wa Habari wa waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbalo amesema kutokana na kuwepo na Mapungufu kwenye katiba iliyopo ndio Maana Serikali imetoa wigo mpana kwa Asasi za kirahia kujadili ili kuweza kuirekebisha na kupata Katiba Nzuri.
“Katiba hii ni Nzuri inafaa ila ina mapungufu, Hata katiba ya Marekani inayo mapungufu lakini huwa inafanyiwa Marekebisho”. Alisema Dk Ndumbalo
Dkt. Ndumbalo ameongeza kumekuwepo na mijadala kuhusu katiba mpya hivyo tunataka katiba ya tano pia tunataka katiba nzuri yenye Marekebisho.
Amesema Katika mchakato huo Serikali imekuwa ikishirikiana vizuri na wadau mbalimbali kutoka nyanja zote ikiwemo Asasi za kiraia.
“Katiba haikuwekei chakula mezani ila inakupa Uhuru kwa hiyo suala kuheshimu katiba ni la kila mtu wanasiasa na wananchi wa kawaida”. Aliongeza Dkt. Ndumbalo.