Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Moraviani Jimbo la Mashariki, Ushirika wa Mbezi Luisi, Mchungaji Timothy Mwankenja akifanya maombi katika ibada Maalamu ya Kusifu, Kuabudu na Maombezi iliyofanyika siku ya jumapili ya tarehe 17/7/2022 katika hilo lililpo Mbezi jijini Dar es Salaam.Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Moraviani Jimbo la Mashariki, Ushirika wa Mbezi Luisi, Mchungaji Timothy Mwankenja akiwaombea wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya ibada Maalamu ya Kusifu, Kuabudu na Maombezi. Ibada hiyo inafanyika kila mwezi katika kanisa hilo.Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Moraviani Jimbo la Mashariki, Ushirika wa Mbezi Luisi, Mchungaji Timothy Mwankenja akiwaombea waumini wa kanisa hilo katika ibada Maalamu ya Kusifu, Kuabudu na Maombezi baada ya kukubali kuoka na kuacha maisha ya kutenda dhambi katika maisha yao.Kwaya ya vijana Kanisa la Moraviani Jimbo la Mashariki, Ushirika wa Mbezi Luisi wakitoa huduma katika ibada Maalamu ya Kusifu, Kuabudu na Maombezi iliyofanyika siku ya jumapili ya tarehe 17/7/2022 katika hilo lililpo Mbezi jijini Dar es Salaam.Baadhi ya waumini wa Kanisa la Moraviani Jimbo la Mashariki, Ushirika wa Mbezi Luisi wakiwa katika maombi katika ibada Maalamu ya Kusifu, Kuabudu na Maombezi iliyofanyika siku ya jumapili ya tarehe 17/7/2022 katika hilo lililpo Mbezi jijini Dar es Salaam. (Picha na Noel Rukanuga).
………………………………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Watanzania wametakiwa kuondokana na utamaduni wa kusali kwa mazoea badala yake wanapaswa kumuabudu Mungu katika roho na kweli jambo ambalo litawasaidia kuepukana na changamoto pamoja na kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Akizungumza katika ibada Maalamu ya Kusifu, Kuabudu na Maombezi iliyofanyika siku ya jumapili ya tarehe 17/7/2022 katika Kanisa la Moraviani Jimbo la Mashariki, Ushirika wa Mbezi Luisi, Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Mchungaji Timothy Mwankenja, amesema kuwa ibada ya kweli ni ulinzi kwa kila mtu anayemwamini Mungu.
Mchungaji Mwankenja, amesema kuwa kumuabudu Mungu ni kuwa na ushirika na yeye katika kuhakikisha unakuna na mawasiliano mazuri kupitia sala na maombi.
Amesema kuwa ukisoma kitabu cha nabii Yohane 3 : 16 kimeeleza Mungu aliacha Mbingu na nchi kwa sababu ya kuwapenda wanadamu, hivyo tumeubwa ili tuwe na ushirika na Mungu.
“Tumeubwa kwa mfano wa sura ya Mungu, tuache kujinenea mabaya, binadamu aliyeubwa kwa mfano wa Mungu anafanikiwa katika jambo lolote, tumuabudu kwa uzuri na utakatifu” amesema Mchungaji Mwankenja.
Amesema kuwa Roho Mtakatifu ni mwaminifu katika maisha yetu ya kila siku, lakini vipo baadhi ya vitu ambavyo tumejiwekea sisi wanadamu katika utaratibu wa kumuabudu Mungu, lakini sio vya kweli mbele yake.
Amesema kuwa tunapaswa kuishi kwa kutumia vipawa vyote ambavyo Mungu amekupa katika maisha yako ili ukifa uwe umetimiza kusudi la Bwana na kutofanya hivyo ni vibaya kwani umeshindwa kutimiza kusudi la lake.
“Mungu ndani yako aliweka maono uwe aidha uwe tajili, ulikomboe Taifa, umiliki viwanda, lakini ukifa bila kuonesha kipawa chako tutalia kuliko msiba wenyewe, na kuwepo duniani bila kumuabudu Bwana aliyekuumba ili umuabudu hiyo ni mbaya kuliko kitu kingine chochote ” amesema Mchungaji Mwankenja.
Mchangaji Mwankenja ameeleza kuwa anatamani kuona kila mtu anamwabudu katika roho ya kweli na kuondoka katika ibada ya maigizo na kuacha kabisa kumuabudu Mungu katika mwili.
Amesema kuwa hakuna kitu ambacho kinaweza kuzuia mkono wa Mungu, hivyo tuna kila sababu ya kujiepusha na mambo yanahusu Mungu katika kuongea kinyume.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Ibada ya Kusifu, Kuabudu na Maombezi, Kanisa la Moraviani Ushirika wa Mbezi Luisi, Dkt. Oswald Masebo, amesema kuwa kupitia ibada ya kusifu na kuabudu ambayo inafanyika mara moja kila mwezi wameendelea kuinuliwa kiimani na kuwa karibu na Mungu.
Dkt. Masebo amesema kuwa ibada hiyo imekusudiwa ili wakristu wapate neema ya kumuabudu Mungu kwa kumsifu, kufanya maombi pamoja na watu wenye shida mbalimbali wapate nafasi ya kuombewa.
“Kuna huduma ya maombezi kwa watu wenye shida mbalimbali kusudi Mungu aweze kushughulika na mahitaji yao ndani ya ibada ya kusifu, kuabudu na maombi” amesema Dkt. Masebo.
Ameeleza kuwa katika ibada hiyo wakristu wamepata nafasi ya kuliombea Taifa, kanisa, familia zao pamoja na kumshukuru Mungu kwa neema ambayo ameendelea kuwapa kanisa hilo pamoja na watu wake.
Dkt. Masebo amefafanua kuwa lengo kubwa la ibada ya kusifu, kuabudu na maombi ni kumtukuza Mungu ili yeye mwenyewe ajitwalie utukufu wake.
“Nimepata neema ya kumtumikia Mungu kama Mwenyekiti wa Kamati ya kuandaa ibada maalumu ya kusifu, kuabudu na maombi, lakini maono anayo Mungu Mwenyewe kwa sababu huduma tunayofanya sio ya kwetu binafsi ni ya Mungu Mwenyewe” amesema Dkt. Masebo.
Amesema kuwa Mungu Mwenyewe anaendelea kuachilia maono na mawazo ya kila mwezi namna ambavyo ibada inapaswa kufanyika.
Ameeleza kuwa wanaendelea kumuomba Mungu kwani ibada hiyo ni dalili za muamusho mkubwa ambao unaendelea kuchukua nafasi katika makanisa mbalimbali.
Hata hivyo waumini wa kanisa la Moraviani Jimbo la Mashariki, Ushirika wa Mbezi Luisi wamemshukuru Mungu kwa maono ya kushiriki ibada ya kusifu, kuabudu na maombezi kutokana imeendelea kuwa baraka katika maisha yao.
Bi. Kumbuka Luwondo amesema kuwa anamshuku Mungu kwa sababu katika ibada hiyo wameona mabadiliko ya kujifunza namna ya kumtumika Mungu, ibada halisi na kusongea katika viwango vya kuomba kwa muda mrefu.
“Tumepata muda mzuri ya kumuabudu Mungu, kusifu na kuabudu na watu pia wamepata nafasi ya kuokoka na kutengeneza maisha yao mpya jambo ambalo katika ibada nyengine sio jambo la kawaida” amesema Bi. Luwondo.
Ibada ya kusifu, kuabudu na maombi Kanisa la Moraviani Jimbo la Mashariki, Ushirika wa Mbezi Luisi inafanyika mara moja kila mwezi katika Kanisa la Moraviani Jimbo la Mashariki, Ushirika wa Mbezi Luisi ambapo waumini wa kanisa hilo wanapata fursa kumuimbia Mungu pamoja na kufanya maombi mbalimbali ikiwemo kuliombea Taifa.