Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda (wa kwanza kulia) akiwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Profesa Boniventure Rutinwa (wa pilikulia) wakizungumza jambo walipokuwa wakiangalia Bidhaa za mbogamboga zilizozalishwa na wanafunzi wa SUA kwenye maonesho ya vyuo vikuu yanayofanyika Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda kushoto na Profesa Boniventure Rutinwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiangalia matunda mbalimbali na mbogamboga zinazozalishwa na wanafunzi wa chuo hicho.
Profesa Boniventure Rutinwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akizungumza jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda alipotembelea banda la chuo cha SUA kwenye maonesho ya vyo vikuu yanayofanyika Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Dkt Nyambilila Amuri Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Dhahada ya Awali (SUA) akizungumza na baandhi ya wanafunzi waliotembelea kwenye banda la chuo hicho katika maonesho ya vyuo vikuu Mnazi Mmoja.
Baadhi ya wanafunzi wakiendelea na Udahili kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine Mkoani Morogoro.
Profesa Boniventure Rutinwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda wakimsikiliza Dkt. Nyambilila Amuri Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Dhahada ya Awali (SUA) walipotembelea banda la chuo hicho kwenye maonesho ya vyo vikuu yanayofanyika Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Profesa Raphael Chibunda (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Chuo hicho kwenye Banda lao katika Maonesho hayo Jijini Dar es Salaam.
Bi. Suzana Magobeko Afisa Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo mkoani Morogoro akifuatilia kwa makini wakati maofisa Udahili wa chuo hicho Mawesa Nicholaus kulia na Grace Kihombo wakiendelea na kudahili wanafunzi katika banda la chuo hicho.
Bi. Suzana Magobeko Afisa Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo mkoani Morogoro akielekeza jambo kwa wakati maofisa Udahili wa chuo hicho Mawesa Nicholaus kushoto na Abel Magembe wakiendelea na kudahili wanafunzi katika banda la chuo hicho.
Bi. Suzana Magobeko Afisa Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo mkoani Morogoro akiwa ameshika moja ya joho lililoshonwa a wanafunzi wa chuo hicho.
………………………………
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Shahada za awali Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) cha mkoani Morogoro Dkt. Nyambilila Amuri amesema kuwa kumekuwepo na muamko mkubwa kwa vijana kutaka kusoma masomo ya ujasiriamali hususani kilimo Biashara. kutoakana na fursa za kujikwamua kiuchumi zilizopo kwenye sekta hiyo.