Balozi wa Uholanzi (Netherlands) nchini Tanzania, Balozi Wiebe De Boer (katika), Mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC Wakili Onesmo Olengurumwa (kushoto) pamoja na Afisa Dawati la Ulinzi la Mtandao, Wakili Paul Kisabo (kulia)
Balozi wa Uholanzi (Netherlands) nchini Tanzania, Balozi Wiebe De Boer (katika), Mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC Wakili Onesmo Olengurumwa.
………………….
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC, umepata ugeni wa kutembelewa na Balozi wa Uholanzi (Netherlands) nchini Tanzania, Balozi Wiebe De Boer.
Balozi Wiebe amefika katika ofisi za THRDC akiambatana na Afisa mkuu wa sera kutoka ubalozi huo, Wakili Chikulupi Kasaka na kufanya mazungumzo na sekretarieti ya Mtandao wa THRDC ikiongozwa na Mratibu, Wakili Onesmo Olengurumwa, pamoja na Afisa Dawati la Ulinzi la Mtandao, Wakili Paul Kisabo.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Afisa Habari, THRDC leo imesema katika ziara hiyo balozi Wiebe amefanikiwa kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na mtandao wa THRDC katika kulinda na kutetea watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania.
Aidha amejadiliana na kujifunza kwa undani kazi zinazofanywa na mtandao, ikiwa ni pamoja na kufahamu hali ya Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania na kuangalia mbinu zinazoweza kutumiwa na Ubalozi huo kuendelea kuboresha na kuendeleza mashirikiano yake na mtandao wa THRDC.
Imeelezwa kuwa kwa muda sasa THRDC imekuwa na mashirikiano ya karibu na ubalozi wa Uholanzi, hiyo ni katika kuhakikisha watetezi wa haki za binadamu wanatengenezewa mazingira salama na rafiki katika utekelezaji wa shughuli za utetezi lakini pia wanalinda na kutetea haki za binadamu nchini.