Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makala ameeleza hayo leo jijini Dar es salaam akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Dar es salaamBaadhi ya viongozi na wadau mbalimba mbalimbali ambao wameshiriki kwenye kikao hicho.
…………………………….
NA MUSSA KHALID
Mkoa wa Dar es salaam umeanzisha mbinu mpya ya ufanyaji wa usafi kwenye barabara zote zinazozunguka mji huo kuanzia July 30 mwaka huu ili kuuweka katika hali ya usafi .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makala ameeleza hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Dar es salaam, wakiwemo Watu wa usalama,Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi,Mameya pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa akitolewa tathmini ya kampeni ya Safisha pendezesha Dar es salaam.
RC Makala ametoa tahadhari kwa viongozi wa serikali za mitaa kujitathmini kwa kutimiza wajibu wao katika kusimamia suala la utunzaji wa Mazingira kwenye maeneo yao ili kulifanya jiji kuwa katika hali ya usafi wakati wote.
Miongoni mwa Barabara kubwa ambazo RC Makalla ameelekeza kufanyiwa Usafi wa Hali ya juu ni Nyerere road, Bagamoyo road, Morogoro road, Mandela Road, Kilwa road, Pugu Road na nyinginezo kwakuwa zinabeba taswira ya Jiji Hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya Mkoa wa Dar es salaam,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James amesema watahakikisha wanayatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa Mkuu wa Mkoa.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge kwa niaba ya Mameya wa jiji hilo,amesema kwa wataendelea kusimamia suala ya usafi katika Manispaa wanazoziongoza.
Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Namoto Yusuph ameishauri serikali kuwashirikisha wamachinga katika kuwa mabalozi wa usimamizi wa mazingira kwani wengi wameonekana kuwa ndo wanaongoza kwa uchafuzi kutoka ufanyaji wa biashara.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema baada ya ujenzi wa soko la Kariakoo kukamilika biashara zitafanyika saa 24.