Mkutano
wa 24 wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala
ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO)
utafanyika jijini Pretoria, Afrika Kusini kuanzia tarehe 16 hadi 19 Julai, 2022.
Mkutano
huo umetanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu unaofanyika tarehe 16 na 17 Julai
2022 ambapo ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kamati hii unaongozwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Fatma M. Rajab ambaye anamwakilisha Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine.
Mkutano
wa 24 unalenga pamoja na mambo mengine kupokea na kujadili agenda mbalimbali zikiwemo mapitio ya
utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa 23 wa MCO na Wakuu wa Nchi na Serikali wa
SADC; Hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya kanda; na tathmini ya hali ya Ulinzi na Usalama katika Kanda pamoja na Tathmini ya athari zitokanazo na mgogoro unaoendelea katika bara la Ulaya.
Viongozi wengine kutoka Tanzania wanaoshiriki
Mkutano wa Makatibu Wakuu ni pamoja na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna
Makakala, Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi,
Lt. Jenerali Salum Othman, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Meja
Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Kamishna wa Polisi Salum Hamduni, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano
wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Agnes Kayola na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga.
Ujumbe
wa Tanzania kwa ngazi ya Mawaziri unatarajiwa kuongozwa na Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye ataambatana na Mhe.
Dkt. Stergomena Tax, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Sehemu ya Ujumbe wa Serikali ya Angola ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu |
Sehemu ya Ujumbe wa Serikali ya Botswana ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu<!–[if gte mso 9]> |