Mhe jaji Mstaafu Robert Makaramba akiwasilisha mada ya wanahari namna ya kuandika na kuripoti habari za kwenye mahakama katika mafunzo kwa wanahabari kuhusu namna Bora ya kuandika habari hasa za Haki za Binadamu ambayo imefanyika Leo Mkoani Morogoro.
Wakili Kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu -THRDC Leopold Mosha akieleza dhumuni la Mtandao Huo kuandaa Mafunzo hayo ambayo yamefanyika Leo Mkoani Morogoro
Afisa Uchechemuzi -THRDC Nuru Maro wakati akiwasilisha mada namna ya Umuhimu wa waandishi wa habari na katika kufanya uchechemuzi.
Picha ya pamoja.(picha na Mussa Khalid)
………………………………
NA MUSSA KHALID, MOROGORO
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando amewataka wanahabari kuendelea kufanya kazi kwa bidii na ueledi zikiwemo za utetezi wa Haki za binadamu Ili kuongeza tija katika kuwahabarisha wananchi taarifa zilizojitokeza na zitakazojitokeza.
Msando amesema hayo leo Mkoani Morogoro wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili kwa wanahabari kuhusu namna Bora ya kutoa habari ambayo yameratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania -THRDC
Aidha Mkuu huyo Wilaya amewataka wanahabari kujitahidi kuwa watetezi wa Haki za Binadamu bila ya kuwa mashabiki wa kuegemea upande mmoja ili kuepukana na changanoto mbalimbali.
Amesema waandishi wa habari wanapozungumza Masuala ya Haki za Binadamu wasiwe wazito kwa kutozitoa badala yake waangalie mzani na ukweli katika kuhabarisha umma Juu tukio wanalotaka kuliripoti.
Naye Mhe jaji Mstaafu Robert Makaramba amewasilisha mada ya wanahabari namna ya kuandika na kuripoti habari za kwenye mahakama kuwa ni vyema wakaepuka kutoa taarifa ambazo hazijatolewa mahakamani ili kuepusha sintofahamu kwenye jamii.
Awali akizungumza Wakili Kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu -THRDC Leopold Mosha amesema Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kuandika ma kuripoti taarifa zinazohusiana na haki za Binadamu.
Wakili Mosha amesema kuwa Moja ya majukumu ya Asasi za Kiraia ni kufanya uchechemuzi wa kujua na kupata ufahamu wa Masuala mbalimbali yanayohusu Haki za Binadamu.
Kwa Upande wake Afisa Uchechemuzi -THRDC Nuru Maro wakati aliwasilisha mada ya Umuhimu wa waandishi wa habari Katika kufanya uchechemuzi kuwa ni Pamoja na kufahamu Chanzo,Ushahidi,kujua Watu wengine wanavyofanya kazi Hilo Eneo husika.
“Ili kuwe na mabadiliko lazima umma uelewe hivyo ni vyema wanahabari mukaonyesha Umuhimu Katika kutoa elimu kuhusiana na Masuala ya Haki za Binadamu Pindi munapoona Kuna ukiukwaji”amesema Nuru
Hata katika mafunzo hayo ambayo ambayo yameanza Leo na yanamalizika siku ya kesho July 13 wanahabari wamesisitizwa kutumia fursa hiyo kujiongezea maarifa katika ufanyaji wao wa kazi.