Mkurugenzi na Tamasha la Ongala Music Festival Aziza Ongala amesema Tamasha la Muziki la Ongala akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la Ongala Music Festival Aziza Ongala litakalofanyika Tar 5-7 Mwezi wa nane Mwaka huu.
Mkurugenzi wa Kituo Cha Utamaduni na Sanaa cha Alliance France Flora akieleza jinsi wanavyowaunga mkono Familia ya Dr Ongala (picha Mussa Khalid)
…………………………
NA MUSSA KHALID
Watanzania wametakiwa kujitokeza Kwa wingi kwenye Tamasha kubwa la Kimataifa la Muziki la Ongala Music Festival 2022 linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Tar 5-7 Mwezi wa nane Mwaka huu ili waweze kujionea burudani yenye vionjo vya kitanzania
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi na Tamasha la Ongala Music Festival Aziza Ongala amesema Tamasha la Muziki la Ongala limejengwa katika Hali ya maadili ya Remmy ya kuwawezesha kuwaweka na kuwasaidia wasanii kote barani Afrika.
Aidha Aziza amesema tamasha Hilo limelenga kutoa Jukwaa la Kimataifa kwa wasanii wa Kiafrika Kwa lengo la kukuza muziki na kukua ndani ya Bara lao Huku wakilenga kufika maono ya Remmy ya kuchanganyia na aina tofauti ya Sanaa za Muziki Nchini.
Amesema Muziki Ongala umekuwa na ujumbe na ujuzi ambao kwa wasanii wa kizazi kipya cha sasa wanaweza kukitumia hivyo amewataka wasanii kutumia fursa hiyo kwa lengo la kujitangaza.
“Enzi za baba kulikuwa hakuna rekodi studio kwani ilikuwa miziki ikipigwa live tofauti na ilivyosasa na kwa Mwaka huu hivyo ujumbe wetu Kwenye Tamasha Hili kwa waka huu ni”Muziki ni tiba”amesema Aziza
Kwa Upande wake Mtoto wa Remmy Ongala ambaye ni mwanamuziki Tommy Remmy Ongala amesema atashiriki katika tamasha hilo kwa ajili ya kuhakikisha linafanikiwa kwa ubora wa viwango.
“Kuna siku kabla Mzee hajaondoka duniani ameshawahi kutuambia kuwa musikubali mziki wangu ukapotea nasi ndo maana kama familia tumeona ni vyema tukawa tunafanya matamasha kama haya ya mara kwa mara kwa lengo la kumuenzi baba”amesema Tommy
Aliko Mwakanjuki ambaye ni Mwakilishi wa Action Music amesema program hiyo itafanyika ndani katika ukumbi wa Serengeti hall na watahusika katika kusimamia mipangilio kufanyika kama walivyopanga.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Kituo Cha Utamaduni na Sanaa cha Alliance France Flora amesema wameamua kushirikia na watoto wa Ongala Ili kuweza kufanikiwa tamasha hilo.
Hata hivyo Imeelezwa kuwa Tamasha Hilo Sasa ni msimu wake wa nne ambapo huadhimishwa Muziki,Maisha na urithi wa Dr Remmy Ongala (1947-2010) Pamoja na Ari na Utamaduni wa watu wa Tanzania.