Waziri wa mifugo na uvuvi,Mashimba Ndaki akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika jijini Arusha .
Kaimu Mkurugenzi wa Muungano wa Afrika kwa rasilimali za wanyama (AU-IBAR) Dk .Nick Nwankpa (kulia)akimkabithi zawadi Waziri wa mifugo na uvuvi, Mashimba Ndaki katika kikao hicho jijini Arusha.
…………………
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mashamba Ndaki amesema kuwa katika kipindi cha miezi sita Tanzania imeuza nyama tani elfu 10 katika nchi za Bara la Asia tofauti na miaka ya nyuma.
Ndaki ameyasema hayo jijini Arusha wakati ya akifungua warsha ya siku saba ya wataalamu wa sekta ya mifugo kutoka nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika{SADC} unaolenga kujadili namna ya kuongeza thamani ya nyama nyekundu yanayotokana na ng’ombe wa asili.
Amesema kuwa, ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika nchini za Bara la Asia hususani nchi za kiarabu limeweza kufungua mwanga kwa nchi hizo kuwa wanunuzi wakubwa wa nyama ya hapa nchini na hadi kufikia desemba mwaka huu huenda Tanzania ikauza nyama nyingi kuliko miaka yote.
Waziri Ndaki amesema kuwa,kutokana na hilo kupitia Wizara yake wamepanga mpango kazi wa kuhakikisha wanafuga mifugo bora yenye lengo la kumpatia mlaji bidhaa bora kwa maslahi ya nchi.
“katika kipindi cha mwaka mzima wa mwaka jana Tanzania iliuza nje ya nchi nyama tani Elfu 7 lakini kwa mwaka huu hali imekuwa tofauti sana kwani katika kipindi cha miezi sita nchi imefanikiwa kuuza nje ya nchi nyama ya kiasi cha tani Elfu 10.”amesema Waziri Ndaki.
Waziri amesema kuwa, kutokana na hali hiyo Wizara imepanga kuboresha sekta ya Mifugo kwa kufuga kisasa katika vituo vyake vya ng’ombe na mbuzi kuwa na mifugo yenye ubora itakayoshindana na soko na huku akiwataka wafugaji kufanya hivyo kwa maslahi ya nchi.
Amesema kuwa, katika kuboresha hilo Wizara imepanga kujenga mabwawa ya Mifugo zaidi katika Mikoa yote yenye mifugo mingi, pamoja na kujenga majosho kwa ajili ya kulinda ugonjwa kwa mifugo.
Waziri Mashimba ameongeza kuwa serikali imepanga kushirikiana na nchi za SADC katika kuboresha mifugo na kuwa na nyama bora kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi kwani nchi za SADC zina mifugo bora kuliko nchini zingine katika Bara la Afrika.
Mtaalamu wa maswala ya teknolojia ,ujuzi na ubunifu katika mradi wa Live2Afrika (AU-IBAR)Dk Mary Kariuki amesema kuwa,wamekuwa na mijadala ya kutosha katika eneo hilo katika kuhakikisha wanaboresha mnyororo wa nyama wa thamani katika eneo la kimazingira katika nchi za ukanda wa SADC.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Muungano wa Afrika kwa rasilimali za Wanyama(AU -IBAR) Dk .Nick Mwankpa amesema kuwa, wataalamu wa nchi hizo watatoka na maazimio yenye tija kwa nchi hizo na kwenda kufanyiwa kazi kwa ajili ya faida ya nchi hizo na sio vinginevyo.
Mwisho